Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mpya Kutoka WhatsApp : Sasa Utaweza Kufuta Meseji Ulizotuma

Sasa utaweza kufuta zile meseji ambazo tayari ulisha zituma kwa watu
DELETE FOR EVERYONE DELETE FOR EVERYONE

Miezi michache iliyopita tulizungumzia sehemu mpya ya WhatsApp ambayo ilitangazwa kuja hivi karibuni ambapo watumiaji wa programu ya WhatsApp wataweza kufuta meseji walizotuma tayari na meseji hizo zitafutika mpaka kwa mtu uliyemtumia. Sehemu hiyo ilikuwa ikiitwa “recall message” kwa wakati huo.

Sasa habari njema ni kuwa sasa sehemu hiyo imesha zinduliwa rasmi na tayari imesha anza kutoka kwa baadhi ya watu na labda kwa siku za usoni watu wote wanaweza kuanza kuitumia sehemu hiyo.

Advertisement

Kujua kama sehemu hiyo imewezeshwa kwako cha kwanza hakikisha una update programu ya WhatsApp na kisha fungua mtu ulie mtumia meseji unayotaka kufuta kisha chagua meseji unayotaka kufuta kisha bofya kisehemu cha kufuta (kitufe cha mchoro wa pipa) kilichoko juu upande wa kulia.

Ukiona umetokea ujumbe huu ‘Delete for everyone’ basi ujue sehemu hiyo imewezeshwa kwenye programu yako ya WhatsApp, lakini kama ukiona meseji imefutika bila kutoa ujumbe wowote basi ujue sehemu hiyo bado haijawezeshwa endelea kuangali update za programu hiyo na kujaribu kwa kufuata maelezo hayo niliyokupa hapo juu.

Endapo utafanikiwa kupata ujumbe huo (ikimaanisha sehemu hiyo imewezeshwa) basi uliyemtumia atoweza kuiona meseji uliyomtumia bali ataona ujumbe huu ‘This message was deleted’ ikimaanisha kuwa meseji hiyo imefutwa na aliyeituma.

Sehemu hiyo mpya inategemewa kusambaa kwa watumiaji wote wa programu ya WhatsApp wa mifumo yote ya iOS, Android pamoja na Windows na inategemewa kuitwa “Delete for everyone”.

Je nini maoni yako kuhusu sehemu hii.. je unadhani watu wanao tumia mitandao vibaya wanaweza kuendelea kutumia vibaya mtandao wa WhatsApp kwa sababu tu sasa watakuwa na uwezo wa kufuta meseji walizo zituma awali..? tuambie maoni yako hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : The Next Web

2 comments
  1. Natumai ni jambo jema sana maana SMS mambazo kilikuwa zipo fasta ukituma ni za WhatsApp so now is solution imepatikana

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use