Hivi karibuni kampuni ya mozilla ambayo ndio watengenezaji wa kisakuzi (browser) cha Firefox wamerudi tena na aina mpya ya kisakuzi kilicho fanyiwa maboresho pamoja na kuongezewa kasi zaidi kinachoitwa “Firefox Quantum”.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo kisakuzi hicho kina kasi zaidi mara sita zaidi ya kisakuzi cha zamani ambacho kilikua kinatumiwa hapo awali, kingine cha ziada ni kuwa kisakuzi hicho kina kasi kuliko hata kisakuzi cha “Google Chrome” kinacho semekana kuwa kwa sasa ndio kinatumiwa na watu wengi zaidi.
Zaidi ya hapo ni kuwa uwezo wa kisakuzi hicho kipya kwa upande wa RAM ni kuwa kinatumia RAM kidogo zaidi ukilinganisha na kisakuzi cha Google Chrome ambacho kinatumia kiasi cha MB 500 au zaidi ya RAM pale unapo kitumia kwenye kompyuta au simu yako lakini hii inategemeana sana na kurasa ulizo fungua kupitia kisakuzi chako.
Kwa sasa kisakuzi hicho kinapatikana kwenye vifaa vyote unaweza kukipata kwenye kompyuta au simu yako ya iOS au Android. Unaweza kudownload sasa kwa kubofya link hapo chini na ujaribu kisha tuambie maoni yako kuhusu kasi na uwezo wa kisakuzi hicho kipya.
- FireFox – Kompyuta
- FireFox – Android
- FireFox – iOS
Nini maoni yako kuhusu kisakuzi hiki kipya cha Firefox unaona kina kasi ile inayotakiwa, na je ni bora kuliko kisakuzi cha Google Chrome..? tuambie kwenye maoni hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.
Iko poa sana ni fasta kinoma
Iko poa sanaaaaaaa