Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Pasaka Hii (2020)

Furahia sikukuu ya pasaka kwa kuangalia movie hizi ukiwa nyumbani
Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Pasaka Hii (2020) Hizi Hapa Movie Nzuri za Kuangalia Pasaka Hii (2020)

Kama wewe ni mmoja wa watu wanao sherekea sikukuu ya pasaka siku ya leo basi ni wazi kuwa unasherekea ukiwa nyumbani kwako, hii ni kutokana na janga la virusi vya corona ambalo linaendelea kuikumba duniani ikiwa na hali ya hewa ya mvua kama ulipo sasa kunanyesha mvua.

Kutokana na hili leo nimekutelea list hii ya movie nzuri ambazo unaweza kuangalia pasaka hii ukiwa nyumbani kwako. Kumbuka unaweza kupakua movie hizo kupitia link chini ya video husika, pia vile vile movie hizi zimechanganyika hivyo unaweza kupata movie za teknolojia pamoja na zile ambazo ni movie nzuri lakini sio za teknolojia. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie movie..

Advertisement

Bloodshot (2020)

Movie hii ni nzuri sana lakini sio moja kati ya movie ambazo unaweza kuangalia na familia, movie hii inayo mapigano ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa sio mazuri kwa watoto chini ya umri wa miaka 13.

Pakua Movie Hapa

Bad Boys for Life (2020)

Movie hii pia sio nzuri kwa watoto, hivyo hii haifai kuangalia na familia au watoto ambao ni chini ya umri wa miaka iliyo elekezwa. Movie hii ina matamshi yasiofaa kwa watoto pamoja na mapigano.

Pakua Movie Hapa

Dolittle (2020)

Movie hii ni nzuri sana kwa familia na inaweza kuangalia pia na watoto na hata watu wazima, movie hii ina mauthui na lugha zinazofaa kwa watoto.

Pakua Movie Hapa

The Call of the Wild (2020)

Movie hii pia ni nzuri kwa watoto na pia unaweza kuangalia na familia nzima, movie ina maudhui ambayo anaweza kuangalia mtoto kulingana na umri ulio tajwa.

Pakua Movie Hapa

Ip Man 4: The Finale (2019)

Movie hii haifai kwa kuangalia watoto kutokana na kuwa na mapigano ambayo yanaweza kuwa sio mazuri kwa watoto chini ya umri wa miaka iliyotajwa.

Pakua Movie Hapa

Underwater (2020)

Movie hii haifai kuangalia watoto chini ya umri uliyotajwa, hii inatokana na movie hii kuwa na scene za kutisha ambazo zinaweza kuwa hazifai kwa mtoto chi ya umri wa miaka iliyotajwa.

Pakua Movie Hapa

Onward (2020)

Movie hii ni nzuri kwa watoto hivyo unaweza kuangalia na familia, movie ina lugha zinazo faa kwa watoto kutokana na umri uliotajwa.

Pakua Movie Hapa

The Hunt (2020)

Movie hii haifai kwa kuangalia na watoto kutokana na kuwa na lugha ambazo hazifai ikiwa pamoja na mapigano ambayo yanaweza kuwa sio mazuri kwa mtoto chini ya umri ulio tajwa.

Pakua Movie Hapa

Journey to China: The Mystery of Iron Mask (2019)

Movie hii pia haifai kuangalia na familia kwa kuwa na mapigano ambayo yanaweza kuwa hayafai kwa namna moja ama nyingine kwa watoto wenye umri chini ya miaka iliyotajwa.

Pakua Movie Hapa

Na hizo ndio movie nzuri ambazo nimekuandalia siku ya leo ya jumapili ya pasaka, kama unataka movie zaidi unaweza kuangalia Movie za kuangalia jumapili hapa. pia kama huna bando la kupakua movie hizi unaweza kusoma hapa kujua mitandao mbalimbali pamoja na bando za bei nafuu ambazo unaweza kupata wenye mtandao wako wa simu. Pia unaweza kujaribu njia hii hapa ya kupata salio bure kwenye mitandao ya simu yako kwa kutumia Dent. Mpaka siku nyingine guys nawatakia wote heri ya siku kuu ya pasaka na mue na afya njema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use