Motorola RAZR ni moja kati ya simu ambazo zilikuwa maarufu sana miaka kadhaa iliyopita hasa kwenye upande wa muziki pamoja na kamera. Well 2019 kampuni mama ya Motorola, Lenovo imetangaza kuhusu ujio wa toleo jipya la Motorola RAZR ikiwa kama ile simu ya Samsung inayojikunja iliyo tangazwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa tovuti ya WSJ, simu hiyo mpya ya Motorola RAZR inategemewa kuzinduliwa rasmi mwezi wa pili mwaka huu na itaanza kupatikana kwanza kwa nchini marekani. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, bado hakuna taarifa zaidi kuhusu sifa za simu hiyo ila inasemekana simu hiyo itakuwa na muonekano tofauti kabisa na simu ya Motorola RAZR ya zamani.
Mwaka 2019 tegemea kuona simu nyingi zinazo jikunja kwani kampuni kama Huawei pamoja na kampuni ya LG zote zimesha tangaza nia ya kuzindua simu zao ambazo nazo zinajikunja mwaka huu 2019. Kwa sasa simu inayo jikunja iliyopo sokoni inatoka kwa kampuni ya Royole ambayo imetengeneza simu ya FlexPai ambayo hiyo ndio simu ya kwanza inayojikunja kuingia sokoni.
Hadi hapo simu hizi mpya kutoka kwenye makampuni makubwa kama Samsung na Huawei zitakapo tolewa rasmi, bado hakuna simu inayo jikunja yenye muonekano mzuri wa kuweza kuingia sokoni na kukubalika na watumiaji. Japokuwa simu ya flexpai ipo sokoni, bado teknolojia yake sio nzuri kama unavyoweza kuona simu hiyo kwenye video hapo juu simu hiyo haina muonekano mzuri na pia hata ukunjikaji wake ni mgumu tofauti na ambavyo tuliona simu ya Galaxy F ilipoonyeshwa kidogo hapo mwaka jana (2018).
Hadi tarehe 20 ya mwezi wa pili itakapo fika nadhani tuendelee kusubiri kuweza kuona teknolojia hii ya simu zinazo jikunja inapoingia sokoni kwa mara ya kwanza ikiwa inafanya kazi vizuri kabisa.