Kila mwaka Apple hufanya mkutano wa WWDC au Apple Worldwide Developers Conference, kwenye mkutano huo Apple hupata nafasi ya kuonyesha bidhaa zake mpya ikiwa pamoja na mambo mengine yanayohusu mifumo mipya ya uendeshaji ya vifaa vya kompyuta na Simu kutoka Apple.
Mwaka huu mkutano huo unafanyika kuanzia siku ya kesho tarehe 4 mwezi huu june na mkutano huo utaendalea mpaka siku ya ijumaa tarehe 8. Ndani ya muda wote huo wa siku 5 tutakuwa tukikuletea matangazo ya moja kwa moja kuhusu yote yatakayo jiri kwenye mkutano huo ikiwa pamoja ni kupitia kwenye ukurasa wetu maalum wa WWDC ambao utakuwepo kwenye tovuti hii kuanzia siku ya kesho.
Kurahisisha mambo uweze kujua nini cha muhimu kwenye mkutano huo siku ya kesho nimekuandalia baadhi ya mambo ambayo yanategemewa kuwepo kwenye mkutano huo ambao unaanza rasmi kuanzia siku ya kesho, basi bila kupoteza muda twende tukangalie mambo hayo.
Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali inasemekana kwenye mkutano huo wa WWDC 2018, Apple inategemea kuonyesha simu mpya ya iPhone SE 2 ambayo ni toleo la maboresho ya simu ya iPhone SE ambayo alizinduliwa March 21, 2016. Lakini bado hakuna taarifa kamili kama simu hiyo itazinduliwa kwenye mkutano huo hivyo ni muhimu kuifuatilia mkutano huo kupitia hapa Tanzania Tech ili uweze kujua zaidi.
- Mfumo Mpya wa iOS 12 na macOS 10.14
Siku za karibuni kumekuwa na tetesi za ujio wa mifumo mipya ya uendeshaji ya vifaa vya Apple, iOS 12 na macOS 10.14 hivyo ni wazi tegemea kusikia kuhusu maboresho mapya ya mifumo hiyo ikiwa pamoja na jinsi mifumo hiyo itakavyo kuwa inafanya kazi.
- Maboresho ya App Store
Kitu kingine kinacho tegemewa ni maboresho ya soko la programu la App store, soko hilo linategemewa kuongezewa muonekano zaidi wa kuwezesha watumiaji na watengenezaji wa programu kutumia soko hilo kwa urahisi.
Programu ya siri inategemewa kuboreshwa zaidi na kuongezewa sauti mpya pamoja na uwezo zaidi wa kufanya kazi kwa ubora zaidi
Na hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaweza kuwepo kwenye mkutano huo wa WWDC 2018, Sasa kupata yote kwa usahihi ungana nasi hapo kesho kwenye ukurasa wetu ambao utakuwa unakupa mkusanyiko wa habari zote kuhusu mkutano huo kuanzia siku ya kesho.
ndg yangu