Kama ilivyo kawaida leo Tanzania Tech tumekukusanyia matukio yote yaliojiri kwenye mkutano mkubwa wa WWDC au Apple Worldwide Developers Conference ambao ulifanyika hapo june 5 siku ya jumatatu mwaka huu.
Kama tunavyojua mkutano huu ni moja ya mikutano muhimu sana kwa watumiaji wa vifaa kutoka kampuni ya Apple, kwani mkutano huu unaonyesha mikusanyiko ya matoleo mapya ya programu mbalimbali za vifaa vya Apple pamoja na kuonyesha baadhi ya bidhaa mpya ambazo Apple huzitoa baadae mwishoni mwa mwaka huo. Kwa mwaka huu kuna matukio sita muhimu ambayo yalitangazwa na Apple na haya ndio matukio yenyewe.. oookey lets get to it…
- tvOS
Kama wewe ni mpenzi wa tvOS ya kutoka Apple kampuni hiyo hapo june tano ilitangaza rasmi kuongeza channel zake kwenye kifaa kicho pamoja na TV App, channel iliyongezwa ni Amazon ambayo itakuwa na Amazon Prime video ambayo tumeona baadhi ya matangazo yake kwenye mtandao wa youtube.
- watchOS
Kama wewe ni mfuatiliaji wa Apple watch kampuni ya apple imetangaza kuwa sasa saa zake zitakuwa zinatumia mfumo mpya wa watchOS 4 ambayo utakuwa na aina mpya ya programu ya siri pamoja na aina mpya ya saa ambayo sasa itaongezewa katuni wengine watatu ili kuleta mvuto zaidi wakati unaangalia saa yako ya Apple Watch.
- Mac
Kwa upana wake hapo june 5 kampuni hiyo ya Apple ilizinduwa mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta za mac ambao umepewa jina la MacOS HighSierra mfumo ambao una maboresho kwa upande wa Safari Browser ambapo imeongezewa baadhi ya vitu vitakavyo fanya utumie intenet bila wasiwasi, Auto Play Blocking ni moja ya sehemu hiyo iliyongeza kwenye kisakuzi cha Safari, kwa kutumia hii unaweza kuzuia video zinazojicheza zenyewe pale unapo peruzi kurasa zenye video mbalimbali. Vilevile pia kisakuzi hicho cha safari kitakuwa na uwezo wa kuzuia matangazo kuangalia vitu unavyopenda kwenye mtandao kwa kutumia sehemu mpya ya Intelligent Tracking Prevention, sehemu nyingine zilizo ongezwa ni Search Top Hit, Split View pamoja na Apple File System. Toleo hilo jipya litapatikana kwenye vifaa vyote vyenye uwezo wa MacOs Sierra na itapatikana bure kabisa.
- Kompyuta za iMac
Kwa upande wa kompyuta za iMac Apple wamefanya mabadiliko kidogo kwa kuongeza prosessor za 7th Genaration Kaby Lake yenye teknolojia za high rate and turbo kwa kutumia teknolojia hii simu yako itaweza kuongezeka nguvu kwa asilimia 50 ikiwa na uwezo wa RAM mpaka GB 16 na Hard Disk Mpaka Terabyte TB 2. Vile vile kompyuta hii ya iMac itaongezewa port mbili za Thunderbolt 3 ambazo zitakuwa sambamba na zile za awali.
- Macbook Pro
Kwa upande wa macbook pia Apple imeongeza prosessor kwenye laptop zake uku ikiwa na uwezo zaidi kwa asilimia 50 uku ikiwa na uwezo wa RAM zaidi pamoja na uwezo wa kusoma kwa Hard Disk kwa haraka.
- Kompyuta Mpya ya iMac Pro
Kampuni ya Apple ikuishia hapo bali ilifanya uzinduzi wa kompyuta yake mpya ya iMac Pro yenye sifa bora na yenye uwezo mkubwa wa graphics kuliko kompyuta zote za apple, pamoja na uwezo wa hali ya juu wa processor. kujua sifa kamili za kompyuta hii mpya pamoja na bei yake tembelea ukurasa huu.
- iOS 11
Kwa wale wanaotumia mfumo wa iOS sasa mfumo mpya wa iOS 11 unakuja na maboresho machache ambayo yamefanyika kwenye iMassege, iPay, Siri, Kamera pamoja na sehemu mpya inayokuja ya Control Center ambayo itakuruhusu kutumia simu yako kwa haraka sana kujua zaidi angalia video hapo juu. Kingine bora kabisa ni programu inayoitwa AR Kit hii ni sehemu mpya kabisa inayokusaidia kutumia kamera ya simu yako kwa namna mpya kabisa kujua zaidi angalia video hapo juu.
- Tablet Mpya ya iPad Pro
Kampuni ya Apple pia ilizindua tablet mpya ya ipad pro yenye ukubwa wa inch 10.5 yenye kutumia kioo chenye teknolojia ya retina uku ikiongezewa teknolojia ya HDR na ikiwa na refresh rate ya 120hz pamoja na processor ya A10X yenye nguvu karibia na laptop ya kawaida, zaidi pia tablet hii inakuja na kalamu ya kukusaidia kutumia tablet yako kama unataka kuchora chochote kwenye tablet yako. vile vile kuna mabadiliko kwenye mfumo wa uendesha kwenye ipad pro kuna programu mpya nyingi pamoja na uwezo mpya wa ku-drag and drop pamoja na malt tasking.
Pia Apple wamezindua App mpya ya File Manager ambayo sasa itakupa uwezo wa kuendesha na kupanga mafile yako yote kupitia App hiyo kujua zaidi angalia video hapo juu.
- Home Pod
Apple pia walitangaza kifaa kipya kinachoitwa Home Pod, kifaa hicho kitakuwa na uwezo wa siri pamoja na uwezo wa kuunganishwa na simu yako au kifaa chako chochote cha Apple kujua zaidi angalia video hapo juu.
Na hayo ndio yote yaliojiri kwenye mkutano wa WWDC ambao ulianza rasmi hapo june 5 siku ya jumatatu, kwa habari zaidi usiache kutembelea Tanzania Tech kila siku ili kupata habari na makala mbalimbali za teknolojia.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.