Habari kubwa siku ya leo, mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Twitter Jack Dorsey, hivi leo ametangaza rasmi kuachia kiti chake cha ukurugenzi kwenye kampuni ya Twitter.
Kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu, Jack Dorsey ametangaza kuwa ameamua kujiuzulu kwa mapenzi yake na uamuzi huu ni mgumu lakini ni uamuzi sahihi kwa wakati huu.
Jack Dorsey ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa Twitter na alikuwa CEO au mkurugenzi mtendaji wa mtandao huo tokeo mwaka 2006, hadi hapo siku ya jana.
not sure anyone has heard but,
I resigned from Twitter pic.twitter.com/G5tUkSSxkl
— jack (@jack) November 29, 2021
Kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu, Jack Dorsey amemteua Parag Agarwal ambaye alikuwa CTO wa kampuni hiyo kuchukua nafasi yake ya CEO. Hata hivyo Jack Dorsey ataendelea kuwa kwenye bodi hadi hapo May 2022 na baada ya hapo ataondoka kabisa kwenye kampuni ya Twitter.
Moja ya sababu ambazo Jack amezitoa ni pamoja na kuamini kuwa Twitter inaweza kujiendesha na hakuna haja ya yeye kama mwanzilishi kuendelea kuongoza kampuni hiyo.
“I believe it’s critical a company can stand on its own, free of its founder’s influence or direction,” alisema Jack Dorsey kwenye email yake ya kujiuzulu.