Kama umekuwa mfuatiliaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii, basi lazima utakuwa unajua kuwa bunge la uganda limepitisha sheria ya kuanza kuwalipisha watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii nchini humo. Mitandao hiyo ni pamoja na Facebook, Twitter, Viber, na WhatsApp.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Quartz Africa, sheria hiyo ilianza kufanyiwa kazi mwezi Aprili baada ya rais wa nchini humo, Yoweri Museveni, kuandika barua kwa hazina ambayo inasema kwamba mitandao ya kijamii inatumika kusambaza uvumi ambayo inapotezea muda na pesa.
Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa leo Julai 1, wananchi wa uganda wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 121 kila siku, sawa na makadirio ya Tsh 44,200 kwa mwaka mzima.