Katika ulimwengu huu wa teknolojia ni muhimu sana kuwa makini na afya zetu kwani mara nyingi vifaa au madini yanayo tumika kutengeneza baadhi ya vifaa hivi vya kiteknolojia hua na madhara makubwa katika mili yetu pamoja na afya zetu kwa ujumla.
Katika kujua hilo leo ni vema nikujuze kuhusu hili la mionzi kwenye simu, najua utakuwa umesha wahi kusikia tetesi nyingi pamoja na habari kuwa simu za mkononi zina sababisha saratani lakini katika hili ni vyema nikueleze kwa undani kidogo ili uweze kuelewa vizuri.
Vifaa vya ndani kama battery ya simu na vinginevyo vimetengenezwa na madini ambayo mara nyingi huwa ni sumu kwa binadamu. Kwa mfano kwenye battery ya simu huwa kuna kemikali mbalimbali ambazo uchanganya na kuweza kufanikisha utengenezaji wa battery.
Kila battery hiyo inapotumiaka utoa kiasi flani cha mionzi ambayo hii huwa sio mizuri kwa afya ya binadamu iwapo ikizalishwa kwa wingi hivyo basi, kwa mujibu wa sheria za nchi mbalimbali vifaa vyote vya kieletroniki vinatakiwa kupimwa kiasi cha mionzi inayotolewa na vifaa hivyo kabla ya kuingia sokoni na hapa ndipo sasa tunakuja kwenye hili neno SAR.
SAR kirefu cheke ni Specific Absorption Rate, hichi ni kipimo cha kiasi cha mionzi inayofyonzwa na mwili wa binadamu (RF energy) pale anapotumia vifaa vya kieletroniki kama vile simu, kompyuta na vinginevyo.
kwa mujibu wa sheria za nchi mbalimbali ni lazima kifaa chochote cha kieletroniki kiwe kimepimwa na kuthibitishwa kuwa kiasi cha mionzi inayotolewa hakina madhara kwa binadmu.
Je utajuaje kiasi cha mionzi inayotolewa na simu yako..?
Kila kampuni ya simu iliyo dhibitishwa kutoa simu za mkononi ni lazima ihakikishe kuwa simu zake zinapimwa kiasi cha mionzi kabla haijaleta simu hizo kwenye soko la watumiaji.
Mara nyingi kampuni zilizo dhibitishwa huonyesha kiasi hicho kwenye simu au kwenye tovuti za simu hizo, sasa basi ili kujua kiasi cha mionzi inayotolewa na simu yako hizi ndio hatua za kufuata.
Kwa Kutumia Code
Kama unatumia smartphone unaweza kubofya kwenye simu yako *#07#, kama umetumia namba hii na ujaona lolote kama mimi basi unaweza kutumia njia ya pili ambayo na uhakika itafanya kazi kwenye simu yako.
Kwa Kutumia Website
Bofya moja ya website kulingana na watengenezaji wa simu kisha ingiza namba ya model ya simu yako kisha utaletewa kiasi cha mionzi inayotolewa na simu yako. Kama utaulizwa nchi na upo Afrika ni vyema kuchagua nchi yoyote iliyopo Afrika kama Nigeria.
Je kiasi gani cha mionzi ni salama
Ili kujua kiwango cha mionzi kwenye simu yako ni salama ni vyema ujue kuwa ni kiwango gani cha mionzi ambayo inatolewa na simu yako ni salama.?
Kwa mujibu wa FCC marekani kiwango kidogo cha mionzi ndio salama kwa mfano kuna simu zina kiasi cha mionzi 1.8 na zingine zinayo 0.6 au hata 0.5 zote hizi ziko salama hivyo ni vyema ukajua kabla ya kununua kifaa chako.
Njia gani zingine za kujilinda
Simu nyingi ambazo azija dhibitishwa huwa na kiwango kikubwa cha mionzi hivyo ni vyema kuacha kutumia simu za kichina ambazo hazina tovuti wala maelezo ya usalama wa afya.
Njia nyingine hakikisha hutumii mara kwa mara simu yako pale inapo pata joto kubwa kwani mara nyingi mionzi hii hutolewa kwa wingi wakati simu ikiwa na joto kali. Hakikisha kuwa unatumia headphone pale unapo ongea na simu kwa muda mrefu.
Mpaka hapo najua utakuwa umepata ujumbe na maarifa jinsi ya kujikinga na mionzi hii inayotokana na vifaa vya kiteknolojia, Je vipi umegundua wewe simu yako inatoa mionzi kiasi gani..? tuambie kwenye maoni hapo chini.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
Simu yangu ni infinix hot 4 ina kiwango cha mionzi 1.6 kwa mafundisho yenu ni salama nawashukuru sana kwa kutuelimisha.Lakini pia naomba msaada nataka ku-install windows kwenye simu yangu moja wapo kati ya Tecno boom j8 au Infinix hot 4 nimepitia hatua zote lakini mwisho inaniambia no butable device,je simu hizi hazina uwezo wa kitu kinachoisaidia kuweka windows?
Sim yangu ni ifinix hot8 Niki itumia hata kwa chini ya dakika3 sikio lina uma kwa ndani sana. Nnini tatiza? Na SAR take ni 1.6?