Kwa wale wapenzi na watumiaji wa simu na vifaa vya Apple, leo ni siku muhimu sana ambapo watu wote duniani wataenda kushudia matoleo mapya ya mifumo ya uendeshaji ya vifaa mbalimbali kutoka kampuni ya Apple.
Kuhakikisha unapata ubora unaotakiwa kampuni ya apple imetangaza kufanya mkutano wake mkubwa uliopewa jina la Apple Worldwide Developers Conference au WWDC ambao utafanyilka kuanzia tarehe 5 mwezi wa sita yaani leo, hadi tarehe 9 mwezi wa sita huko mjini San Francisco nchini marekani.
Katika mkutano huo Apple inatarajiwa kutoa mfumo mpya wa iOS toleo la 11 ambalo litaongezewa baadhi ya vitu pamoja na kutoa ubora zaidi kwa vifaa vyote vinavyotumia mfumo huo, vilevile kampuni ya Apple inatarajiwa kutoa mfumo mpya wa kompyuta zake za Macbook ambapo taarifa zinasema kuwa mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa pamoja na mamboresho ya laptop moja kutoka kampuni hiyo, bado hakuna taarifa zaidi kuhusu ni laptop gani itakayo fanyia maboresho lakini usiwe na wasi wasi kwani taarifa zote utazipata hapa baada ya mkutano huo kufanyika hapo baadae.
Kingine kipya ni kuwa tegemea kuona aina mpya za programu kwenye soko la App Store kwa mfumo wa iOS, programu hizo zitakuwa zinatumika sambamba na mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 11 ambao utazinduliwa hapo baadae kwenye mkutano huo wa WWDC 2017. Pia kama utataka kuangalia tukio hilo LIVE au Mubashara kabisa unaweza kufanya hivyo kwa kubofya Link Hapa, kumbuka tu ni lazima kuwa na kisakuzi cha Safari au kama unatumia kompyuta unaweza kutumia kisakuzi au browser ya Microsoft Edge.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.