Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Microsoft Yazindua Kompyuta Mpya ya Desktop Inayoitwa Surface Studio

Microsoft kwa mara nyingine tena imezindua kompyuta mpya aina ya Desktop kwenye familia ya kompyuta za Surface PC
Surface Studio Surface Studio

Familia ya kompyuta za aina ya surface zinazo tengenezwa na kampuni ya Microsoft leo imeongezeka rasmi baada ya kampuni hiyo kuzindua kompyuta mpya aina ya desktop ya Surface Studio. Kompyuta hiyo imezinduliwa leo kwenye mkutano uliofanywa na kampuni ya Microsoft huko mjini New York nchini marekani.

Katika Uzinduzi huo kiongozi anaeongoza timu ya engineer kutoka katika kampuni hiyo ya microsoft Panos Panay alisema “tunamini kuwa kompyuta mpya ya Surface Studio itabadilisha jinsi watu wanavyo tengeneza, wanavyo buni na wanavyo jifunza” kiongozi huyo aliendelea kusema “kompyuta ninayo enda kutambulisha leo itaonekana kama imefanana na nyingine lakini itakuwa na uwezo wa tofauti” alimalizia kusema kiongozi huyo na kisha akatambulisha kompyuta hiyo.

Advertisement

Kompyuta hiyo mpya ya Surface Studio ina fanana kidogo na kompyuta ya desktop kutoka kampuni ya Apple iMac, lakini kompyuta hiyo inasemekana kuwa na kioo cha LCD chembamba pengine kuliko kompyuta nyingine ya desktop duniani, Ikiwa na upana wa 12.5mm tu sawa na inch 0.492126 ikiwa imewezesha na touchscreen kompyuta hiyo aina ya desktop ina kava la aluminum kwa nyuma huku kioo cha kikionyesha output ya pixels milioni 13.5 ambayo ni sawa na zaidi ya asilimia 63 ya kioo cha televisheni ya 4K kinavyo onyesha.

Kompyuta hii mpya ya Surface Studio ina uwezo mkubwa wa kuonyesha rangi vizuri hvyo inafaa zaidi kwa photographers, videographers, na designers Microsoft wenyewe wanaita kompyuta hiyo”True Color”. Rangi pamoja na kioo cha kompyuta hiyo zinaendesha na Graphics Card ya Nvidia GTX 980M GPU ambayo ni moja ya Graphics card ambayo inafanya vizuri sana, pia kompyuta hiyo inauwezo wa kulala kwa nyuma kioo chake karibia na kuwa flat kabisa ili kukupa uwezo wa kutumia touchscreen ya kompyuta hiyo.

Pia kompyuta hiyo inauwezo wa kutumia peni maalum pamoja na kifaa kipya ambacho unapokilaza kwenye kioo cha kompyuta hiyo unauwezo wa kurekebisha rangi, sauti pamoja na vitu vingine. Kompyuta hiyo itakuwa ikiuzwa kuanzia dollar za marekani $2,999 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 6,549,666.05 ili Kujua zaidi kuhusu sifa kamili za kompyuta hii endelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech.

Nini maoni yako kuhusu kompyuta hii mpya kutoka Microsoft tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use