Microsoft Yazindua Kompyuta Mpakato Mpya za Surface Book 2

Sasa zimeongezwa nguvu zaidi pamoja na Battery yenye uwezo mkubwa
Microsoft Surface Book 2 Microsoft Surface Book 2

Kampuni ya Microsoft hivi karibuni imetangaza toleo jipya la kompyuta mpakato (Laptop) zake mpya za Surface Book 2, Laptop hizi zimekuja na muundo mpya, uwezo mpya wa battery, nguvu zaidi pamoja na kuongezewa ukubwa na kwa sasa laptop hizi zinatoka kwa aina mbili tofauti.

Advertisement

Kwa muundo laptop hizi ni sawa na toleo lililopita lakini utafauti uliopo ni kuwa sasa laptop hizi zinapatikana kwa aina mbili nchi 15 pamoja na inch 13.5, Laptop hizo zote zinauwezo wa kuwa laptop na tablet huku zikiwa na uwezo wa kutenganishwa kioo kama ilivyo laptop mpya ya HP Zbook x2.

Kwa upande wa sifa laptop hizi zote zinaendeshwa na processor 7th generation Intel ‘Kaby Lake’ processors lakini pia unaweza kupata yenye processor za 8th generation Intel ‘Coffee Lake’ processors.

Kwa upande wa graphics Surface book 2 ya inch 13.5 ina graphics ya Intel HD Graphics 620 (Kaby Lake) na pia inapatikana ikiwa na graphics nyingine za Intel UHD Graphics 620 (Coffee Lake) au NVIDIA GeForce GTX 1050 zote zikiwa na uwezo wa GB 2. Surface Book 2 ya inch 15 inakuja na graphics ya Intel UHD Graphics 620 au NVIDIA GeForce GTX 1060 zote zikiwa na uwezo wa GB 6.

Laptop zote mbili zinakuja na aina tatu za ukubwa wa Hard Disk yaani GB 256, GB 512 pamoja na  Terabyte TB 1 zote zikiwa zinapatikana pia kwa teknolojia ya Solid State Storage  huku zikiwa  zinasaidiwa na RAM ya GB 8 au GB 16 DDR3.

Kwa upande wa USB laptop hizi zote mbili zina USB-A 3.0 ports, port moja ya USB-C port, SD slot, headphone jack pamoja na Surface connector, Microsoft inasema laptop hizi zinadumu na chaji kwa masaa 17 ukiwa una angalia video na kwa masaa 5 ukiwa unaitumia kama tablet (yaani umeitengenisha na keyboard).

Surface Book 2 zinakuja na zikiwa na price tag ya dollar za marekani $1499 kwa laptop ya inch 13.5 ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 3,300,000 wakati laptop ya inch 15 ikiwa na bei ya dollar za marekani $2499 sawa na shilingi za Tanzania Tsh 5,620,000. Bei hizi ni kwa mujibu wa viwango vya fedha vya leo hivyo kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Na hizo ndio laptop mpya za Microsoft Surface Book 2 zilizo zinduliwa hivi karibuni na kama kawaida tungependa kusikia maoni yako, vipi bei za laptop hizi zinaendana na muundo na sifa ulizosoma hapo juu..? Tujulishe kwenye maoni hapo chini… Pia usisahu kuodownload App ya Tanzania Tech kwa habari zaidi za teknolojia.

Chanzo : Windows Blogs

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use