Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Microsoft Yaja na Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Ofisini

Sasa fanya mikutano kwa kutumia Microsoft’s Surface Hub 2
Microsoft Yaja na Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Ofisini Microsoft Yaja na Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Ofisini

Hakuna kitu cha muhimu kama unapokuwa ofisini kuwa na uwezo wa kuonyesha wafanyakazi wenzako kile unacho kifikiria tena hasa pale anapokuwa mbali na mkutano wenyewe. Kuliona hilo, kampuni ya Microsoft inakuja na Microsoft Surface Hub 2. Hii ni aina mpya ya kompyuta yenye muonekano kama ubao ambayo itakuwa inatumika kwenye ofisi kwaajili ya kufanya mikutano mbalimbali.

Advertisement

Microsoft’s Surface Hub 2 inakuja na kioo cha inch 50.5 chenye teknolojia ya 4K pamoja na Aspect Ratio ya 3:2 huku ikiwa na kingo ndogo sana za pembeni kama inavyo-onekana kwenye video hapo juu. Microsoft’s Surface Hub 2 inaruhusu wafanyakazi kuitumia kwa kuiwasha kwa fingerprint, huku kamera yake yenye uwezo wa 4K ikikupa uwezo wa kupiga simu za video huku ukiona kama uko pembeni ya unaye mpigia simu hiyo.

Mbali na hayo Microsoft Surface Hub 2 inakupa uwezo wa kuunganisha kioo hicho na vioo vingine kama hivyo ili kukupa uwezo zaidi wa kufanya mikutano ukiwa ofisini kwa namna ya kipekee. Kompyuta hiyo itakuwa inatumia mfumo wa uendeshaji wa Windows 10 na utakuwa na uwezo wa kunganisha Microsoft Surface Hub 2 na laptop yako au kompyuta yenye mfumo wa Windows.

Kwa upande wa Bei bado kampuni ya Microsoft haijatangaza bei halisi ya kompyuta hiyo lakini kutokana na toleo la kwanza la kompyuta hiyo kuuzwa bei ghali, basi ni sawa kusema kuwa Microsoft Surface Hub 2 haitokuwa bei rahisi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use