Inawezekana kabisa kampuni ya Microsoft imeachana na utengenezaji wa simu za mkononi, lakini kwa upande wa tablet kampuni hii bado ina mawazo ya kuja na tablet mpya na zenye ubora unaotakiwa. Hivi karibuni kampuni hiyo imedhirisha hayo kwa kuja na tablet yake mpya ya inch 10 ya Surface Go.
Tablet hii ya Surface Go inakuja na mfumo wa Windows, kioo chenye Aspect ratio ya 3:2 na resulution ya 1800 x 1200 pixel, na kwa mujibu wa Microsoft hii ndio tablet ya Surface nyembamba zaidi na inakuja na uzito wa gramu 520.
Kwa upande mwingine, Tablet hii inakuja na processor ya Pentium Gold 4415Y ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 4 au GB 8 huku kwa upande wa ukubwa wa ndani Surface Go inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 128 zote hizi ikiwa ni SSD. Tablet hii inakuja ikiwa inatumia Wi-Fi pakee na baadae inasemekana kuja na toleo lenye uwezo wa LTE au 4G.
Tablet hii inakuja na mfumo wa Windows S lakini pia inasemekana unaweza kuweke mfumo mzima wa Windows 10. Surface Go inakuja na price tag ya dollar za marekani $399 sawa na TSh 908,000 kwa tablet yenye ukubwa wa ndani wa GB 64 na RAM ya GB 4. Surface Go yenye GB 128 na RAM ya GB 8 yenyewe itauzwa kwa dollar za marekani TSh $549 sawa na Tsh 1,248,000. Kwa sasa tablet hizi hazijaingia sokoni rasmi lakini inategemewa kuanzia mwezi wa nane mwaka huu 2018.