Kampuni ya kubuni teknolojia mbalimbali ikiwemo teknolojia za magari pamoja na vifaa vya muziki vya ndani kutoka nchini marekani Harman, imeingia kwenye ushirikiano na kampuni ya Microsoft ili kutengeneza speaker janja (smart speaker) zinazotegemewa kutoka mwaka 2017.
Katika tangazo lake lilotumwa leo kwenye mtandao wa youtube Microsoft imeonyesha kuwa smart speaker hizo zitakuwa zikitumia programu janja ya Cortana ambapo utaweza kuambia speaker hiyo kufanya vitu mbalimbali, kama vile kuplay nyimbo flani, kukumbusha safari na mambo mengine.
Speaker hizo ambazo zitatengenezwa na kampuni ya Harman kupitia sehemu ya kampuni hiyo ya Harman Kardon, Microsoft itakua ni kampuni nyingine iliyofuata nyayo za kampuni ya Amazon baada ya kampuni hiyo kutoa kifaa kama icho cha Amazon Echo na baadae kufuatiwa na kampuni ya Google iliyokuja na kifaa kama hicho cha Google Home kilichotoka mapema mwaka 2016.
Bado mpaka sasa haijajulikana kifaa hicho kipya kitatoka siku gani na kitakuwa kinauzwa bei gani, mpaka hapo itakapo tangazwa, endelea kutembelea Tanzania tech ili kujua yote kuhusu kifaa hichi kipya kutoka kampuni ya Microsoft na Harman Kardon.
Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.