Kampuni ya Microsoft ambayo ndio watengenezaji wa mfumo wa uendeshaji wa Windows hivi leo imetangaza rasmi kusitisha mfumo wa uendeshaji wa Windows Vista. Ni miaka kumi sasa imepita tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo wa uendeshaji ambao leo umetangazwa kufikia mwisho wake
Katika ukurasa wake wa forum ya msaada Microsoft iliandika kuwa hadi kufikia tarehe 11 ya mwezi April mfumo huo wa uendeshaji hauto pokea tena update zozote au marekebisho yoyote ikiwemo pia programu zozote za bure au za kulipia kutoka kampuni hiyo ya microsoft. Hata hivyo watumiaji wenye mfumo huo wa Windows Vista wata endelea kutumia mfumo huo lakini hawato weza kupata update zozote mpya za programu hiyo.
Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa mfumo huo ni vyema ukaamua kubadilisha mfumo huo kwani kutoka na Microsoft kutokana na mfumo huo kusitshwa utakuwa ni rahisi kushambuliwa na wadukuzi, hivyo chukua hatua ya mapema sasa, download toleo jipya la windows 10.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.