Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Microsoft Yathibitisha Kutaka Kununua TikTok kwa Marekani

Microsoft inategemea kumaliza mazungumzo ya kununua TikTok baada ya Mwezi
Microsoft Yathibitisha Kutaka Kununua TikTok kwa Marekani Microsoft Yathibitisha Kutaka Kununua TikTok kwa Marekani

Siku chache zilizopita (Ijumaa) Raisi wa Marekani aliwambia waandishi wa habari kuwa anategemea kufungia mtandao wa TikTok kutotumika nchini Marekani ndani ya kipindi cha muda mfupi ujao.

Lakini wakati huo huo, kampuni ya Microsoft nayo ilisemekana kuwa ipo kwenye mazungumzo na kampuni ya Byte Dance ili kununua mtandao wa TikTok kwa upande wa Marekani.

Advertisement

Habari mpya zinasema kuwa, kampuni ya Microsoft imethibitisha kuwa ipo kwenye mazungumzo na kampuni hiyo ya China, ili kuweza kununua mtandao wa TikTok kwa upande wa Marekani. Hata hivyo inasemekana kuwa maongezi hayo yanatakiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja ambao Raisi wa Marekani ametoa ili kuruhusu kampuni ya Microsoft na Byte Dance kufikia makubaliano.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, inasemekana kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Microsoft Satya Nadella, aliongea na Raisi wa Marekani siku chache zilizopita na kupewa muda huo wa il kuweza kufikia makubaliano na kampuni ya Byte Dance.

Mbali na marekani, inasemekana kuwa kampuni ya Microsoft imetuma maombi kwa kampuni ya Byte Dance ili kuweza kununua mtandao huo kwa upande wa Canada, Australia, na New Zealand.

Hiyo inafanya kampuni ya Byte Dance ambayo ndio mmiliki wa mtandao wa TikTok kuendelea kumiliki mtandao huo kwa upande wa Afrika pamoja na Ulaya.

Hata hivyo kupitia tovuti ya Microsoft, kampuni ya Microsoft imeainisha kuwa pale itakapo fanikiwa kununua mtandao huo kwa upande wa marekani data za watumiaji wote wa marekani zitakuwa zikihifadhiwa nchini Marekani, endapo kuna data za wamarekani ambazo zilikuwa zikihfahiwa nje ya nchi zita hamishiwa marekani na kufutwa kwenye server hizo ambazo zipo nje ya marekani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use