Teknolojia inaendelea kukuwa sana, kiasi kwamba hata sehemu ambazo zilikua hazihitaji teknolojia basi sasa zimeanza kuweka teknolojia mbalimbali. Kuthibitisha maneno hayo hivi karibuni kampuni ya KFC imeadhimisha miaka 30 ya kutoa huduma za chakula huko nchini china na kuamua kuzindua smartphone yake.
Katika maadhimisho hayo kampuni hiyo ya KFC imeungana rasmi na kampuni maarufu ya kutengeneza simu ya Huawei ili kutengeneza simu hiyo janja ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya kusindikiza kusherekea miaka 30 ya migahawa hiyo huko nchini china.
Simu hiyo ambayo inakuja na rangi nyekundu ikiwa na picha ya utambulisho ya KFC pamoja na mwaka ambapo migahawa hiyo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza huko nchini China. Kuhusu sifa za Simu hiyo ya KFC inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 32 huku ikiwa na programu nyingi zenye kuweza kurahisisha huduma za mgahawa huo nchini humo.
Baadhi ya programu hizo ni pamoja na programu ya kukusaidia kuagiza kuku mbalimbali kutoka kwenye mgahawa huo pamoja na programu ya kukusaidia kuchagua aina gani ya mziki unaotaka kusikia unapokua kwenye mgahawa huo. Hata hivyo bado kampuni ya KFC haija tangaza lini simu hiyo itangia sokoni na kwa bei gani lakini habari kutoka mitandao mbalimbali zinasema huenda simu hiyo ikaanza kuuzwa huko nchini china kupitia mtandao maarufu wa Alibaba.
KFC sasa imekua ni moja kati ya mghawa mkubwa sana duniani na hivi sasa unaonekana kuanza kutumia sana teknolojia kutoa huduma zake mara baada ya hivi karibuni kutangaza kuleta teknolojia ambayo itaweza kutambua chakula unachotaka kula kwa kuangalia hali sura yako.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.