Mgahawa wa KFC wa nchini china hivi karibuni unategemea kufunga mitambo maalum ambayo itaweza kugundua unachokitaka hata kabla ya wewe kuagiza. Mitambo hiyo itaweza kugundua aina ya chakula unachotaka kwa kuangalia jinsia yako, umri wako pamoja na sura yako.
Kampuni ya KFC imeungana na kampuni ya Baidu ili kufanikisha hilo kwenye migahawa yake ya nchini huko. Wakieleza jinsi mtambo huo unavyofanya kazi wataalum kutoka kampuni ya Baidu wanasema kuwa mtambo huo hutumia programu maalum za facial recognition ili kuweza kujua jinsia yako umri pamoja na hali yako ya uso (Face expression) kwa muda huo, kisha kwa kutumia vitu vyote hivyo programu hiyo hutoa maoni au kukuchagulia chakula ambacho kinaweza kukufaa kwa muda huo.
Mfano wa Teknolojia hiyo ni ule wa kwenye filamu ya Minority Report ambayo imechezwa na muingizaji Tom Cruse, kwenye filamu hiyo kunaonekana tayari dunia imeshakua na teknolojia ya hali ya juu kiasi kwamba ukipita kwenye shopping mall matangazo yanaweza kujua jina lako pamoja na kitu gani unachotaka, hata unapoingia kwenye maduka ya nguo matangazo hayo pia huweza kujua kile unachofikiria kununua Angalia video hiyo hapo chini.
Kama teknolojia ndio huku inaelekea ama kweli watu watakua wavivu kufanya mambo ya kawaida hata kuagiza chakula..? Kuogeza zaidi kampuni hiyo ikifanikiwa na hayo pia inatarajia kuwezesha watu kuagiza chakula kwa kutumia selfie. Yaani unapiga picha kwenye simu yako kisha unatuma alafu unaletewa chakula ambacho kinakufaa kwa wakati huo kutokana na picha yako.
Kwa habari zaidi kama hizi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku, au unaweza kudownload programu ya Tanzania Tech kutoka Play Store, pia unaweza kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kupitia Youtube Channell yetu.