Hivi leo habari zimelipuka kwenye kila mtandao zikisema kuwa mfumo wa MacOS High Sierra ambao unatumika kwenye kompyuta nyingi za Apple umegunduliwa kuwepo na tatizo la ulinzi ambalo mtu yoyote atakuwa na uwezo wa kuingia (login) kwenye kompyuta yako kama admin bila ya kuwa na password au nywila.
Kupitia mfumo huo mpya wenye toleo la macOS, version 10.3, mtu yoyote ataweza kuingia kwenye kompyuta yako kwa kuandika neno “Root” kwenye sehemu ya Username na kisha sehemu ya Password huna haja ya kuandika chochote. Kwa kubofya kitufe cha Unlock mara mbili utapata uwezo wa kuingia kwenye kompyuta yoyote yenye mfumo huo mpya wa uendeshaji.
Tayari kampuni ya Apple imetangaza kuwa imesha pata taarifa za tatizo hilo na sasa ina andaa update za kuweza kurekebisha mfumo huo. Kwa sasa watu wote wanao tumia mfumo huo wanapaswa kufuata hatua hizi ambazo zimetolewa na kampuni hiyo ili kuweka ulinzi wa muda huu wakati Apple ikifanyia marekebisho mfumo huo.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.