Pamoja na uzinduzi wa simu mpya za iPhone 15, pamoja na iPhone 15 Pro kampuni ya Apple pia imetengaza kuzindua rasmi mfumo wa iOS 17 ambao ni mfumo wa maboresho wa iOS 16.
Kwa mujibu wa Apple mfumo wa iOS 17 ambao ulikuwa kwenye majaribio kwa muda, hivi karibuni kuanzia September 18 (Mwezi huu wa Tisa), mfumo huu utapatikana kama update au sasisho kwa watumiaji wote wenye simu za iPhone zenye uwezo wa kupokea mfumo huo mpya.
iOS 17 inapatikana kwenye simu zote za iPhone kuanzia iPhone XS na kwenda mbele, hii ina maanisha kuwa simu za iPhone X na kushuka chini zote hazitoweza kupokea mfumo huo mpya.
Mfumo wa iOS 17 unakuja na maboresho mbalimbali, ikiwa pamoja na maboresho kwenye upande wa app ya kupiga simu (Phone App) ambapo sasa utaweza kutengeneza picha maalum itakayo onekana unapo pigiwa simu.
Pia kwa upande wa Siri imeboreshwa zaidi na sasa huna haja ya kusema Hey siri ili kufungua programu hiyo ya Sauti, bali sasa utasema Siri na moja kwa moja utaendelea kwa kusema unachotaka.
Mabadiliko Mengine ni kwenye app ya Maps ambayo sasa inauwezo wa kuonyesha ramani bila kutumia Internet. Pamoja na sehemu mpya ya Check In ambayo itaruhusu kumjulisha mtu pale ulipo kwa kutuma ramani ya ulipo ikiwa na meseji yenye ujumbe wa mahali ulipo.
Mbali na hayo mabadiliko mengine ni kwenye sehemu mpya ya Namedrop ambayo itaruhusu kushare mawasiliano yako kwa kugusanisha simu za iPhone.
Mabadiliko mengine ya iOS 17 ni pamoja na Live Voicemail ambayo itakuwa inaandika ujumbe wa mtu anao uwacha pale anapokutana na Voicemail. Mabadiliko mengine ya mfumo huu unaweza kuangalia video hapo chini.