Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Dell Yaja na Mfumo Mpya wa Dell Cinema kwaajili ya Filamu

Teknolojia hii itaweza kufanya kompyuta ya dell kuwa bora kwenye filamu
Mfumo wa Dell Cinema Mfumo wa Dell Cinema

Ni wazi kuwa wengi wetu tunapenda kuangalia filamu au movie, lakini ni wazi kuwa ni watu wachache sana wanaopenda kuangalia filamu kwenye kompyuta, pengine hii ni kutokana na kutokuwa na kompyuta bora zenye mfumo ulio tengenezwa maalumu kwaajili ya kuweza kuangalia filamu au movie kupitia laptop au Desktop. Ndio maana kampuni ya Dell inakuletea mfumo wa Dell Cinema.

Advertisement

  • Mfumo wa Dell Cinema Color

Tukianza na upande wa mfumo wa Dell Cinema Color kompyuta zenye mfumo huu zitakuwa na programu maalum ya Cinema Color software, Programu hii inafanya rangi za filamu kuwa kama vile za mfumo wa HDR au 4K hata kama filamu haija rekodiwa kwenye mfumo huo au hata kama kompyuta yenyewe haina teknolojia ya 4K, Vilevile ukitumia kompyuta yenye mfumo wa Cinema Color kuangalia filamu kwenye mtandao wa Netflix utaweza kuangalia filamu zile zenye ubora wa HDR10 au Dolby Vision standards hata kama kompyuta yenyewe haina viwango hivyo.

  • Mfumo wa Dell Cinema Sound

Tukihamia kwenye Mfumo wa Dell Cinema Sound kompyuta zitakazokuwa na mfumo huu zitakuwa na programu maalumu ya Waves MaxxAudio® Pro boosts ambayo hii inasaidia kuweza kufanya kompyuta hizo kuwa na uwezo mzuri sana wa sauti wa kisasa na wa kipekee. Mbali na hayo dell wameweka mfumo wa Smart Amplifiers ambao utaweza kuzuia Spika za kompyuta zenye mfumo huo kuharibika kutokana na sauti kubwa.

  • Mfumo wa Dell Cinema Stream

Hatua ya mwisho Dell inakuletea Mfumo wa Dell Cinema Stream, mfumo huu utakuwa maalum kwaajili ya kuangalia filamu au kuangalia video mubashara au Live Streaming. Kompyuta zitakzaokuwa na mfumo huu zinakuja na teknolojia mpya inayokuwezesha kuangalia video bila kukata kata. Kompytuta hizi zime tengenezwa na teknolojia bora ya Wi-Fi pamoja na teknolojia ya SmartByte ambayo itaweza kukupa uwezo mzuri sana wa kuangalia video au nyimbo za mubashara bila kukata kata pale unapotumia kompyuta zenye mfumo huu.

Mifumo hii yote ni maalum kwa kompyuta za Dell na tayari imeshatoka rasmi toka mwezi wa kwanza mwaka huu 2018, baadhi ya kompyuta mpya za Dell za mwaka huu tayari zinakuja na mfumo hiyo, hivyo wakati mwingine unapoenda kununua laptop au kompyuta ya Dell unaweza kuangalia kama inayo teknolojia hiyo ya Dell Cinema kulingana na mahitaji yako.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use