Kampuni ya Google hivi karibuni ilitangaza ujio wa mfumo mpya wa Android 13, hadi sasa yapo mambo mengi ya muhimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu mfumo huu mpya ambao unategemewa kuanza kutumika rasmi kwenye smartphone nyingi kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022.
Kuliona hili leo nimeona nikuletea baadhi ya mambo ambayo utegemee kuyakuta kwenye mfumo huo mpya wa Android 12 pale simu yako itakapo pokea sasisho rasmi baadae mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka 2023. Basi baada ya kusema hayo twende kwenye makala hii.
Mabadiliko ya ulinzi pamoja na sera mbalimbali za faragha ndio mambo yaliyopewa kipaumbele kwenye mfumo huu mpya wa Android 13.
TABLE OF CONTENTS
Muonekano
Kwa kuanza pengine nikufahamishe kuwa mfumo mpya wa Android 13 ndio mfumo ambao unakuja na mabadiliko machache sana ya muonekano kuanzia kulinganisha na mfumo wa Android 12. Hii ni kwa sababu mabadiliko mengi yaliyofanyika ni mabadiliko ya mfumo wenyewe na sio muonekano.
Lakini pamoja na hayo yapo mambo machache ambayo hadi sasa yana muonekano wa tofauti na tukianza na sehemu ya notification.
Mabadiliko hayo ni wakati unasikiliza muziki, kupitia music player sasa utaweza kuona mstari wenye mawimbi mawimbi tofauti na mstari ambao umenyooka. Mstari huu ni ule unao onyesha nyimbo imefikia wapi. Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo chini.
Ni vizuri kujua kuwa mstari huu huonekana hivi iwapo nyimbo au audio yoyote itakuwa ina play bila hvyo mstari huo uwa umeonyooka kama ilivyo awali.
Rangi Zaidi Kupitia “Material You”
Mbali na sehemu ya Notification, Google pia imeongeza rangi zaidi kupitia “Material You” na sasa utaweza kuchagua rangi zaidi.
Mbali na hayo mabadiliko mengine ni machache na unaweza kuangalia mabadiliko hayo kupitia video hapo chini. Kumbuka hili ni toleo la majaribo la kwanza yaani Android 13 Beta 1 na mabadiliko zaidi yanaweza kuwepo kwenye matoleo mengine ya mfumo huu.
Mengine ya Muhimu
Kama kutakuwa na mengine usikose kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech hapa kwani ni wazi kuwa lazima tutaongelea kuhusu mfumo huu mpya wa Android 13.
Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua kuhusu mfumo wa Android 12 ikiwa pamoja na baadhi ya sifa zake. Kama ni mtumiaji wa iPhone unaweza kusoma hapa mabadiliko muhimu kwenye mfumo wa iOS 16.