Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu za Android Zitakazopokea Mfumo Mpya wa Android 10

Hizi ni baadhi ya simu ambazo zitapata mfumo huo mpya
Simu za Android Zitakazopokea Mfumo Mpya wa Android 10 Simu za Android Zitakazopokea Mfumo Mpya wa Android 10

Kampuni ya Google imatangaza ipo kwenye hatua za mwisho za kutoa mfumo mpya wa Android 10, mfumo ambao wote tunajua unakuja na mabadiliko makubwa ikiwa pamoja na mabadiliko ya majina pamoja na mfumo mzima wa Android.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia list ya simu za Android ambazo zinasemekana kupokea mfumo huo mpya wa Android 10 ndani ya Miezi michache inayokuja. Kumbuka list hii ni simu za awali hivyo inawezekana kabisa list hii kuongezwa kadri siku zinavyokwenda. List hii ni kwa mujibu wa tovuti ya Digital Trend ambayo ilifanya mawasiliano na kampuni husika kujua simu zitakazo pata mfumo huo mpya wa Android 10 ambao awali ulikuwa unajulikana kama Android 10 (Q).

Advertisement

Simu za Google Zitakazopata Android 10

Mara nyingi Google hupenda kusasisha toleo jipya la Android kwenye simu zake kwanza kabla ya simu nyingine. Kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu za Google yaani Google Pixel basi habari njema kwako kwani simu hizo nyingi kama sio zote zinategemewa kupata mfumo huo mpya wa Android 10.

Simu za Honor Zitakazopata Android 10

Kampuni ya Honor ambayo ni sehemu ya kampuni ya Huawei nayo pia imetaja list ya simu ambazo ndio zitakuwa za awali zitakapo pata mfumo mpya wa Android 10. Najua wote tunajua mgogoro wa kibiashara wa Huawei na serikali ya marekani lakini pengine tuendelee kusubiri kujua hatma ya kampuni ya Huawei kuendelea kutumia mfumo wa Android.

Simu za HTC Zitakazopata Android 10

HTC ni moja kati ya kampuni ambazo kwa mwaka huu zimekuwa kimya sana na pengine inawezekana kampuni hii ikafikia mwisho kwenye biashara ya simu isipofanya mabadiliko ya haraka. Lakini pamoja na hayo kampuni hiyo pia imetaja simu zake zitakazo pata mfumo huo mpya.

  • HTC U12 Plus
  • HTC U11 Plus
  • HTC U11
  • HTC U11 Life
  • List inaongezwa….

Simu za Huawei Zitakazopata Android 10

Kama unajiuliza sana kama simu yako ya Huawei itapokea mfumo mpya wa Android 10 basi usiwe na wasiwasi kwani marekani imetoa kibali kingine kwa Huawei kuendelea kutumia mfumo wa Android kwa miezi mingine miwili, hii inatoa mwanya kwa Huawei kutoa mfumo huo mpya kwa watumiaji wake. Kama unayo simu hizi basi habari njema kwako.

Simu za LG Zitakazopata Android 10

LG ni moja kati ya kampuni ambayo inatoa simu bora sana hasa kwenye upande wa kioo, simu zote za LG ambazo zinakuja na sifa bora hasa kwenye upande wa Kioo zitapata mfumo huo mpya wa Android 10. Simu hizi ni chache tofauti na ambavyo ungedhani.

Simu za Motorola Zitakazopata Android 10

Motorola ni kampuni ambayo inajitahidi sana kwa sasa kutoa simu mpya na pengine uwenda kampuni hii pia ikawa ndio kampuni ya itakayotoa simu nyingi zitakazo pata mfumo mpya wa Android 10. Zifuatazo hizi hapa ndio simu za Motorola zitakazo pokea mfumo mpya wa Android 10.

Simu za Nokia Zitakazopata Android 10

Nokia ni moja kati ya kampuni ambazo zinafanya come back kubwa sana, kampuni hii inakuja na simu bora za bei nafuu ambazo watu wengi wanaonekana kuzipenda sana. Kama ilivyo kampuni ya Motorola, kampuni ya Nokia pia inasemekana kuwa inategemea kutoa simu nyingi za Android zenye mfumo huo mpya wa Android 10. Zifuatazo ni simu za Nokia zitakazopata mfumo mpya wa Android 10, kumbuka simu zilizo andikwa 2020 basi hizo zitapata mfumo huo mwanzoni au kwenye robo ya pili ya mwaka 2020.

Simu za One Plus Zitakazopata Android 10

One Plus nayo pia haiko nyuma kwenye kutoa mfumo mpya wa Android 10 kwenye simu zake, kupitia simu zake za One Plus hizi hapa ndio simu za Android zitakazo pata kwenye mfumo huo mpya wa Android 10.

Simu za Samsung Zitakazopata Android 10

Najua watu wengi ndio watakuwa wanasubiri list hii hivyo kama unasubiria list hii ni vyema ujue kuwa siku hizi samsung haina mtindo maalum inayotumia kutoa masasisho ya matoleo mapya ya Android. Lakini hizi hapa ndio simu ambazo mpaka sasa zinasemekana kupata mfumo mpya wa Android 10, kumbuka list hii inaweza kuongezeka.

Simu za Sony Zitakazopata Android 10

Sony pia inategemea kutoa mfumo wa Android 10 kwenye simu zake hivi karibuni, japokuwa kampuni hii haina simu nyingi sana za Android lakini hizo chache pia zinategemewa kuboreshwa kwa mfumo huo mpya wa Android 10.

Simu za TECNO Zitakazopata Android 10

Mpaka sasa najua unajua baadhi ya simu zitakazopata mfumo wa Android 10, lakini ni vyema kukumbushana kupitia hapa. Zifuatazo ndio simu za TECNO zitakazo pata mfumo mpya wa Android 10, kumbuka list hii inaweza kuongezeka.

Simu za Infinix Zitakazopata Android 10

Kwa upande wa kampuni ya Infinix ambayo nayo pia ni sehemu ya kampuni ya Transsion Holdings pamoja na kampuni ya TECNO, pia mambo sio tofauti sana kwani inategemewa simu nyingi mpya za Infinix zilizotoka hivi karibuni ndio zitaweza kupata mfumo huo mpya wa Android 10. Kumbuka simu hizi ni baadhi tu ya simu hizo hivyo hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu.

Na hizo ndio baadhi tu ya simu ambazo zinasemekana kuwa zitapokea mfumo huo mpya wa Android 10. Kama hujaona simu yako hapa usijali kwani huwenda list hii ikaongezeka mara baada ya kampuni husika kujaribu mfumo huo kwenye baadhi ya simu zao. Hakikisha unaendelea kutembelea ukurasa huu ili kupata habari zaidi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use