Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mfumo Mpya wa macOS 10.13.5 Haya Ndio Mabadiliko Mapya

Sasa unaweza kusasisha toleo jipya la macOS kwenye kompyuta yako ya Mac
mfumo mpya wa macOS 10.13.4 mfumo mpya wa macOS 10.13.4

Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta yenye mfumo wa macOS basi ni vyema nikakujuza kuwa Apple wametoa toleo jipya la mfumo huo wa uendeshaji kwa ajili ya kompyuta za Mac. Mfumo huo mpya unakuja na maboresho machache kama ilivyokuwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa iOS 11.4.

Maboresho makubwa yaliyopo kwenye mfumo wa macOS 10.13.5 ni pamoja na uwezo wa kuhifadhi meseji kwenye iCloud ambapo utaweza kuona meseji zako kwenye vifaa vyako vyote ikiwemo sasa na kompyuta za Mac. Mbali na hayo utaweza kuhifadhi meseji hizo na endapo utanunua kifaa kipya cha Apple chenye uwezo wa iMessage, basi utaweza kurudisha meseji zako zote kwenye kifaa hicho na meseji zako zitarudi kama kwenye kifaa chako cha awali. Hata hivyo, hayo yatakuwa yanawezekana endapo unatumia Apple ID moja kwenye vifaa vyako vyote.

Advertisement

Mbali na hayo maboresho mengine ni pamoja na maboresho ya ulinzi, ambayo yamefanyika kwenye programu ya Mail App ambayo ilikuwa inaruhusu wadukuzi kusoma barua pepe zilizofichwa, Vilevile Apple pia imeweka ulinzi kwenye app ya iBooks ambayo likuwa inaruhusu wadukuzi kutumia programu hiyo bila kuweka password. Mbali na uboreshaji hayo, Toleo hilo jipya la MacOS High Sierra pia imepokea maboresho kadhaa ya kuongeza ubora na ufanisi.

Toleo hilo jipya la mfumo wa macOS 10.13.5 sasa linapatikana kwenye kifaa chako unaweza kusasisha toleo hilo jipya kwenye kifaa chako sasa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use