Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mfumo Mpya wa iOS 11.4 Haya Ndio Mabadiliko Mapya

Sasa utaweza kuhifadhi meseji zako kwenye iCloud
iOS 11.4 iOS 11.4

Kama wewe ni mtumiaji wa simu au kifaa chenye kutumia mfumo wa iOS basi ni vyema ukajua kuwa mfumo mpya wa iOS 11.4 tayari uko hewani na sasa unaweza kusasisha toleo hilo jipya kwenye simu yako au kifaa chako.

Kama ilivyokuwa kwenye mfumo wa iOS 11.3, toleo hili pia halina mabadiliko makubwa sana, lakini pia kuna baadhi ya vitu ambavyo nadhani ni muhimu kuviangalia. Moja kati ya mabadiliko ya muhimu kwenye toleo hili la iOS 11.4 ni pamoja na uwezo wa kutumia iCloud kwenye sehemu ya meseji. Kama wewe ni mtumiaji wa simu za iPhone sasa utaweza kuhifadhi (Backup) meseji zako kwenye iCloud, ikiwa pamoja na uwezo wa kuzirudisha meseji zako pale unapo nunua au kubadilisha kifaa kipya.

Advertisement

Vilevile sehemu hiyo itakuwa inasaidia kuhifadhi meseji zako na utaweza kuziona kwenye vifaa vyako vyote unavyo tumia iMessage pamoja na iCloud. Ili kuwasha sehemu hiyo kwenye simu yako ya iPhone au iPad, unatakiwa kubofya sehemu ya Settings, kisha gusa jina lako alafu bofya iCloud kisha washa sehemu ya Messages.

Kama wewe unatumia kompyuta ya Mac, unatakiwa kubofya programu ya iMessage kwenye kompyuta yako kisha kwenye menu bar, chagua Messages alafu Preferences kisha bofya akaunti alafu bofya kiboksi kilichopo pembeni ya maneno Enable Messages in iCloud.

Maboresho mengine ni pamoja na toleo jipya la Airplay 2, ambayo hii ni muhimu sana kwa wale wenye spika za homepod ambao wanamiliki spika zaidi ya moja. Airplay 2 itawasaidia kuweza kusikiliza muziki kwenye spika zaidi ya moja kwa mara moja. Yaani kama una spika mbili za Homepod unaweza kusikiliza muziki kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye spika zote mbili.

Na hayo ndio maboresho mapya kwenye mfumo wa uendeshaji wa iOS 11.4, kwa sasa tayari mfumo huu uko hewani na unaweza kupakua toleo hilo jipya lenye takribani MB 300. Kujua zaidi kuhusu mfumo huu unaweza kutembelea ukurasa Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use