Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Haya hapa mambo mapya yanayo tarajiwa kwenye mfumo wa Android 11
Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11 Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Kampuni ya Google tayari imeanza kufanyia kazi mfumo mpya wa Android 11, ikiwa ni takribani zaidi ya mwaka mzima tokea kampuni hiyo ilipo zindua mfumo wa Android 10 mfumo ambao sasa unaendelea kufikia simu mbalimbali za Android kote duniani.

Kwa sasa Android R ndio jina la mfumo huo mpya wa Android 1, mfumo ambao kwa sasa upo kwenye hatua za awali za majaribio. Kwa siku ya leo nitaenda kuongelea baadhi ya sehemu mpya ambazo zipo kwenye mfumo huo mpya ambao unategemewa kutoka rasmi baadae mwaka huu.

Advertisement

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Kwa sababu mfumo wa Android 11 kwa sasa upo kwenye hatua za awali za majaribio, baadhi ya sehemu ambazo zipo kwa sasa zinaweza kuwa zimeboreshwa zaidi, au nyingine zimeondolewa kabisa pale mfumo huu utakapo zinduliwa rasmi. Kwa kusema hayo twende moja kwa moja tukangalie sehemu hizi.

Chat Bubbles

Chat Bubbles hii ni sehemu ambayo ilikuwa kwenye mfumo wa majaribio wa Android 10 lakini hapo baadae Google iliamua kuondoa sehemu hiyo pale mfumo huo ulipo zinduliwa rasmi. Google imeamua kurudisha sehemu hiyo na kama ulikuwa hujui kuhusu sehemu hii inafanana sana na sehemu ambayo inapatikana kwenye Facebook Messenger.

Sehemu hii inaruhusu kuchat na watu mbalimbali kupitia sehemu maalum (bubble) ambayo hufunguka juu ya application yoyote na kuruhusu uweze kuchat bila kufunga programu uliyokuwa unatumia awali kabla ya kupokea meseji hiyo.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Ili kuwasha sehemu hii, pale unapo pokea meseji kutoka kwa mtu kupitia sehemu ya juu ya simu yako ya Android, unatakiwa kuishikilia meseji hiyo kwa muda kama sekunde moja na moja utaletewa sehemu za kuchagua zenye kuonyesha sehemu ya kuwasha bubble ambayo itaruhusu meseji kuwepo juu ya programu yoyote uliyokuwa unatumia awali.

Inasemekana sehemu hii itakuwa inafanyakazi kwenye programu zote za kuchat ikiwa pamoja na sehemu ya meseji za kawaida au (SMS).

Sehemu za Ruhusa Zimeboreshwa

Kama unavyojua hivi karibuni Google imekuwa ikiondoa programu nyingi sana kwenye soko lake la Play Store, hii ni kutokana na kuwa programu hizo nyingi hazifanyi kazi kama zilivyo tarajiwa na badala yake hutumika kuchukua data za watumiaji mbalimbali bila ruhusa.

Kutokana na hili, kwenye mfumo wa Android 11 Google inatarajia kuleta sehemu mpya ya ruhusa ambayo inafanya mtumiaji kuchagua kutoa ruhusu kwenye app mara moja tu na baada ya kumaliza kutumia app hiyo ruhusu hiyo huondolea. Kwa mfano, kama umeruhusu app kujua mahali ulipo utatoa ruhusa hiyo mara moja tu pale unapotumia app hiyo na utakapo funga app hiyo app hiyo hatoweza kujua ulipo mpaka utakapo ifungua tena baadae na kutoa ruhusa.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Sehemu Mpya ya Kurekodi Kioo (Screen recorder)

Kwa watumiaji wa simu za iPhone najua watakuwa wanajua kuwa unaweza kurekodi unachokifanya kwenye simu yako na kushiriki na watu bila kuongeza programu yoyote kwenye simu yako. Sasa kupitia mfumo wa Android 11, Google inakuja na sehemu ya kurekodi kioo cha simu yako moja kwa moja bila kuongeza programu yoyote kwenye simu yako.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Muda wa Kuwasha Muonekano wa Giza (Dark Mode)

Kwenye Android 10 Google ilitangaza ujio wa muonekano wa Giza au Dark Mode, kwa sasa muonekano huu unapatikana kwenye simu nyingi ikiwa na sehemu ya kuwasha na kuzima muonekano huo. Lakini kwenye Android 11, Google inaongeza sehemu mpya ya Automatic Dark Mode sehemu ambayo ina kuwezesha kupata muonekano wa giza kwa muda maalum bila kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Kwa mfano ukiwasha sehemu hiyo ya Automatic Dark Mode, kila saa moja usiku simu yako itakuwa inabadilika yenyewe na kuwa na muonekano wa giza.

Kuzima Notification Wakati wa Kutumia Programu Nyingine

Kupitia Android 11, sasa utaweza kuzima Notification wakati unatumia programu nyingine. Kwa mfano kama unatumia programu ya WhatsApp na umewasha sehemu hiyo mpya ya Do not Disturb kwenye programu hiyo. Moja kwa moja sehemu hiyo itazuia meseji zote za WhatsApp na nyingine kuingia kama notification pale unapotumia programu hiyo.

Yaani ukiwasha sehemu hii kwenye programu maalum, kila mara unapo tumia programu hiyo simu yako itazimwa notification na notification zote hazitotoa milio pale meseji zinapo ingia kwenye simu yako.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Chagua App ya Kushare Vitu Zaidi

Kama wewe ni mtumiaji wa App ya Tanzania Tech, ukiwa unasoma makala ndani ya app hiyo na kubofya kitufe cha kushare makala ndani ya App utaweza kuona app mbalimbali zimeonekana ili kuruhusu wewe kushare makala kwenye app hizo.

Kupitia kwenye mfumo wa Android 11, utaweza kuchagua ni app gani iweze kuonekana pale utakapo chagua sehemu ya kushare kwenye app yoyote. Kwa sasa huwezi kuchagua na inakubidi kutafuta app unayotaka kushare nayo pale unaposhare link au kitu chochote kutoka app moja kwenye app nyingine.

Google Yatangaza Ujio wa Mfumo Mpya wa Android 11

Na hizo ndi baadhi tu ya sehemu ambazo ni muhimu kwenye mfumo wa Android 11, kama unataka kuendelea kujua zaidi kuhusu sehemu nyingine zinazokuja kwenye mfumo wa Android 11 hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kujua zaidi.

Simu Zinazo Pokea Mfumo wa Android 11 wa Majaribio

Kwa sasa kama unataka kujaribu mfumo huu kwenye simu yako unaweza kutembelea tovuti ya Android Developer na utaweza kupata maelezo ya jinsi ya kuweke mfumo huo kwenye simu yako. Hadi sasa simu zinazo weza kupakia mfumo huo wa majaribio ni simu zilizopo kwenye list hapo chini.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use