Mwanzoni mwa wiki hii, kampuni ya Facebook ilitangaza ujio wa sehemu mpya ambayo inaruhusu watumiaji wa programu hiyo ya mawasiliano kuweza kutuma meseji ambazo zinajifuta zenyewe baada ya siku saba kuanzia meseji ilipotumwa.
Sehemu hiyo mpya ambayo tayari imesha anza kupatikana kwa watumiaji wote wa programu ya WhatsApp na pia inaweza kuwashwa kupitia magroup na hata kwa mtu mmoja mmoja.
Pale mtu anapo washa sehemu hii, meseji zote ambazo atakuwa anatuma kuanzia siku aliyowasha sehemu hiyo hadi inapo fika siku saba zitakuwa zinajifuta moja kwa moja. Aidha kupitia blog ya WhatsApp, facebook imeanisha kuwa meseji ambazo zitakuwa mtu na “quote” zitaendelea kuonekana kama kawaida.
Pia kupitia magroup, Admin pekee ndio atakayeweza kuendesha sehemu hiyo ambayo pia itakuwa inafuta meseji zote watu walizochat ndani ya siku saba mara baada ya kuwasha sehemu hiyo.
Kama unataka kuwasha sehemu hii, unachotakiwa kufanya ni kufungua programu yako ya WhatsApp, kisha chagua jina la mtu au akaunti ya mtu au u naweza kuingia kwenye chat yako wewe na mtu huyo kisha bofya profile ya mtu huyo na utaweza kuona sehemu hiyo ya Disappearing Messages. Bofya hapo kisha bofya Continue, kisha chagua On au Off.
Kwa sasa sehemu hii imeanza kupatikana kwa watumiaji mbalimbali huku ikitegemewa kufikia watumiaji wote duniani siku za karibu. Sehemu hii inapatikana pia kwa watumiaji wa simu zote yaani Android pamoja na iOS.
Kama bado hujaona sehemu hii kwenye programu yako ya WhatsApp basi hakikisha una update programu ya WhatsApp kupitia Play Store na App Store.
Kujua zaidi maujanja jinsi ya kutumia programu ya WhatsApp unaweza kusoma hapa.