WhatsApp ni moja kati ya programu ambayo inafanyiwa mabadiliko mengi sana, siku za karibuni tumesikia WhatsApp ikiongezewa kupengele cha Stickers ambapo sasa utaweza kuwasiliana kwa kutumia njia mpya kabisa ya Sticker.
Lakini kama haitoshi siku chache baadae kampuni ya Facebook kupitia app yake ya WhatsApp inasemekana kuwa inategemea kuleta sehemu mpya kabisa kwaajili ya kutuma na kupokea meseji za siri. Sehemu hii ambayo nayo pia inasemekana imenakiliwa kutoka kwenye app ya Snapchat, inakupa uwezo wa kutuma meseji za siri ambazo hazikai kwa muda mrefu.
Kwa wale wanao tumia app ya Snapchat lazima mtakuwa mnajua sehemu ya ephemerality, sehemu hii inakupa uwezo wa kutuma meseji, picha au video ambayo hupotea baada ya muda mfupi mara baada ya mtu kufunga ukurasa aliokuwa anatumia. Lakini kwa upande wa WhatsApp sehemu hii ni tofauti kidogo kwani inasemekana kupitia sehemu hiyo mtu ataweza kutumia meseji kama kawaida lakini meseji hiyo itajifuta baada ya muda fulani kutokana na mtumaji alifvyoseti yeye mwenyewe.
Facebook imekuwa ikiendelea kuchukua vitu mbalimbali kutoka kwenye app ya Snapchat, Siku za karibuni Instagram iliongezewa sehemu kama hii ambayo inakuwezesha kutumia picha au video ambazo zinaweza kupotea mara baada ya kumaliza kuziangalia.
Kupitia app ya Instagram sehemu hiyo inapatikana kama unataka kumtumia mtu picha au video kupitia sehemu ya DM. Kama unataka kutumia picha na video zinazopotea kwenye app ya instagram, ingia kwenye DM yako kisha chagua kitufe cha kamera kisha piga picha au chagua picha kisha chagua View Once, na kisha chagua unaemtumia na baada ya hapo picha hiyo au video itaweza kujifuta mara baada ya mtu uliye mtumiak kuangalia.
Kwa upande wa WhatsApp bado hakuna taarifa za lini sehemu hii itakuja kwenye programu ya WhatsApp au itakuwa inafanya kazi kwa namna gani. Kwa taarifa zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tuta kuhabarisha juu ya ujio wa sehemu hii na jinsi inavyofanya kazi.
asanteni kwa taarifa bora na za uhakika