Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows

Sasa pokea meseji na ujumbe wowote kwenye simu yako ya Android
Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows

Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta yenye mfumo wa Windows 10 pamoja na simu ya Android basi habari njema kwako kwani sasa utakuwa na uwezo wa kupokea taarifa (Notification) za simu yako moja kwa moja kwenye kompyuta yenye mfumo wa Windows 10.

Kwa mujibu wa taarifa kupitia tovuti ya The Verge, hivi karibuni kupitia toleo jipya la App ya Your Phone ya Microsoft utaweza kupokea jumbe ambazo zinatokea kwenye simu yako ya Android moja kwa moja kwenye kompyuta yako ya Windows. Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo ili kuwezesha sehemu hiyo inakubidi kuwa na toleo jipya la App ya Your Phone Companion ya Android pamoja na toleo jipya la app ya Windows 10 ya Your Phone.

Advertisement

Hatimaye Sasa Pokea Taarifa za Simu ya Android Kwenye Windows

Mbali na hayo pia utaweza kusoma na kutuma meseji kwenye simu yako kupitia kompyuta yako ya mfumo wa Windows, vilevile utaweza kuona picha mbalimbali ambazo umepiga muda mfupi uliopita huku ukiwa na uwezo wa kuamisha mafile kutoka kwenye kompyuta yako kwenda kwenye simu kwa urahisi zaidi.

Kwa sasa kama unataka kuwezesha sehemu hii inakubidi kupakua toleo jipya la App ya Your Phone, kisha baada ya hapo pakua app ya Android ya Your Phone Companion kupitia link hapo chini, hakikisha una install app zote kikamilifu kwenye kompyuta yako na kwenye simu yako ya Android kisha fuata maelezo na moja kwa moja utaweza kuunganisha kompyuta yako ya Windows 10 pamoja na simu yako ya Android na kupata taarifa zote za simu yako.

Link to Windows
Price: Free

Kama njia hii unaona ni ngumu kwako, basi unaweza kutumia njia nyingine ya kuweza kuunganisha simu yako ya Android na kompyuta yoyote ambapo unaweza kuendesha simu yako nzima kwa kutumia kompyuta yako, unaweza kusoma makala hiyo hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use