Hivi sasa matumizi ya Smartphone au simu kwa ujumla yamekuwa kwa kasi sana duniani kote, Kuongezeka huku kwa matumizi ya simu pia kunaongeza aina mpya ya uchafu unao tokana na mabaki ya simu zilizotumika, ndio maana kamati ya maandalizi ya mashindano ya michezo ya Olympics 2020 wamekuja na njia ya kupunguza mabaki hayo ya simu zilizotumika.
Kama unavyojua michezo ya Olympics inatagemewa kuanza rasmi mwaka 2020 huko nchini Tokyo, Japan, Japo kuwa bado zaidi ya miezi nane hadi michuano hiyo kuanza rasmi ila tayari habari mbalimbali kuhusu michezo hiyo zimeshaanza kuzuka mtandaoni. Hivi karibuni tovuti ya habari ya theguardian ya nchini marekani imebainisha kuwa, medali zitakazo tumika kwenye michuano hiyo ya Olympics 2020 zitakuwa zimetengenezwa kwa mabaki ya simu zilizotumika.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, baadhi ya vifaa vya ndani ya simu hizo vimetengenezwa kwa madini mbalimbali kama vile gold (dhahabu), silver (silva), pamoja na bronze, madini ambayo pia hutumika kutengeneza medali hizo ambazo watapewa washindi wa michezo tofauti kutoka nchini mbalimbali.
Hadi kufikia mwezi November mwaka jana (2018), tayari zilikuwa zimekusanywa zaidi ya tani 47,488 za simu zilizotumika ambayo ni sawa na simu zaidi ya milioni 5 zilizo kusanywa kutoka miji mbalimbali nchini Japani.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa kamati ya maandalizi ya Olympics 2020, hadi kufikia sasa tayari imeweza kukusanya zaidi ya asilimia 90 ya kiasi cha Gold kinachotakiwa, ambacho ni kilo 30.3kg kwa ujumla, na asilimia 85 ya silver ambayo kwa ujumla ni kilo 4,100kg, huku kwa upande wa bronze ikiwa imekamilisha asilimia 100 ya kiwango kilichokuwa kinahitajika ambacho ni kilo 2,700kg.
Kwa sasa bado zoezi la kukusanya mabaki ya simu zilizotumika linaendelea hadi hapo itakapo fikia tarehe 31 ya mwezi wa tatu mwaka huu 2019, ambapo zoezi hilo litasitishwa na baadae kufatiwa na kutangazwa kwa muonekano wa medali hizo hapo mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu 2019.