Kwa wale wapenzi wa mchezo wa computer na playstation wa Need for speed hii ni habari njema kwenu kwani kampuni inayo husika na utengenezaji wa mchezo huo hivi majuzi imetangaza kuwa mchezo huo unarudi tena ukiwa ni toleo lake la saba toka ilipoanza hapo mwaka 1998.
Watengenezaji wa game hiyo the franchise waliandika katika website yao kuwa toleo hilo jipya litaitwa “Taking Stock: Under the Hood #7,” ambapo tayari mchezo huo umeshanza kutengeneza kwa kutumia maoni ya wapenzi wa game hiyo kote duniani. Hata hiyo the franchise iliongeza kuwa itakua ikialika watu mbalimbali katika office zake ili kutoa maoni mbalimbali yahusuyo utengenezaji wa game hiyo maarufu.
Hivyo basi! kama wewe ni mpenzi wa mchezo huu kaa tayari kwa NFS 7 ambayo inategemewa kuwa kali zaidi ya ile iliyotoka mwaka jana.
Kumbuka endelea kupitia blog ya Tanzania tech ili upate habari zaidi na info za game mbalimbali duniani.
Naisubiri kwa hamu sana hii gemu tafadhali endelea kutufaamisha
Nikweli sanaa hii blog ni ya kweli sana