Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia muda mwingi kukaa ukiwa nafanyakazi kwa kutumia kompyuta basi makala hii ni yako. Pia kama unatumia simu kwa muda mrefu ukiwa umekaa sehemu moja basi makala hii inaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.
Kupitia makala ya leo nitaenda kuonyesha mazoezi maalumu ambayo ni bora kwako wewe mtumiaji wa kompyuta wa muda mrefu, mazoezi haya hayaitaji wewe kutoka mahali ulipo kwani unaweza kuyafanya hapo hapo ulipo bila kujali kama ni ofisini au eneo lako la kazi.
Basi bile kuendelea kupoteza muda wako wa kufanya kazi basi moja kwa moja twende kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Mazoezi ya Mabega
Ukiwa kwenye sehemu yako ya kazi, simama kisha geuza viganja vyako vya mikono kwa nyuma na mikono yako kisha moja kwa moja anza kusogeza mikono yako nyuma kidogo kidogo, fanya hivyo mikono yako ikiwa imeonyooka na fanya kwa angalau sekunde 20.
Squat za Kiti
Ukiwa kwenye kitu chako cha kazini simama kisha funga mikono yako miwili kwa pamoja kisha fanya Squat ambapo sasa utakuwa unaenda hadi karibu ya kukaa kwenye kiti chako, fanya squat hizo angalau kumi au ishirini. Usifanye nyingi sana usije kutoka majasho! haah..
Mazoezi Miguu
Simama kwenye dawati lako la kazi kisha shika kwa mikono yako miwili kisha endelea kwa kuinua mguu wako mmoja huku ukiupeleka nyuma na rudia kufanya hivyo kwa mara ishirini kisha badilisha upande na rudia hatua hizo hizo kwenye mguu mwingine.
Nyoosha Mwili
Ukiwa kwenye kiti chako cha ofisini simama nyuma ya kitu hicho kisha shika kwenye sehemu ya kuegamia ya kiti hicho, kisha moja kwa moja simama kwa vidole huku ukijisogeza mwili juu, rudia tena ukipanda juu na kushuka chini. Rudia mazoezi hayo kwa mara ishirini au zaidi, kumbuka usifanye mara nyingi sana
Nyoosha Kiuno
Kama kwenye ofisi yako kunacho kiti cha kuzunguka basi unaweza kufanya mazoezi haya kwa mtindo huu, kama hakuna basi unaweza kujizungusha mwenyewe kwa upande mmoja kwenda mwingine kwa kuzungusha mikono yako kwenda upande mmoja kwenda mwingine.
Nyoosha Shingo
Ukiwa umekaa kwenye kiti moja kwa moja zungusha shingo yako taratibu kwenda kushoto na kulia ukiwa umeegamia kwenye kiti chako, fanya hivyo taratibu usije kujiumiza shingo yako.
Nyoosha Mabega
Najua hii watu wengi hufanya bila kujua kama inasaidia sana mwingili hasa kwa watu wanao kaa kwa muda mrefu. Unaweza kufanya hii kwa kurudia kwa muda mfupi.
Nyoosha Mgogo na Kifua
Funga mikono yako kwa nyuma kisha sogea kwa mbele huku ukitanguliza kifua kwa mbele, jinyooshe kadri uwezavyo ila kuwa makini na usifanye kwa nguvu sana.
Nyoosha Mgogo wa Juu
Nyoosha mikono yako usawa wa masikio yako kisha inamaa, kadri unavyo inama nyoosha mikono yako zaidi. Inama migono yako ikiwa ukwenye usawa wa masikio huku kichwa kikiangalia chini. Kwa hivyo kwa sekunde tatu hadi nne. Kuwa makini usilale sana utajiumiza.
Nyoosha Mgogo kwa Kiti
Kama kiti chako kinayo sehemu za kushikia basi zoezi hili litakuwa rahisi zaidi, kama huna kiti chanye mikono basi unaweza kufanya hivyo kwa kuzungusha mikono kwa upande mmoja na kurudia kwa upande mwingine.
Na hayo ndio mazoezi ambayo unaweza kufanya kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta wa muda mrefu sana. Kumbuka pia mazoezi haya yanaweza kufanywa kwa mtu yoyote ambaye anakaa kwa muda mrefu sana.
Pia kumbuka kufuata sheria ya 20 20 20 kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta wa muda mrefu, unaweza kusoma hapa kujua zaidi kuhusu sheria hiyo.
Mazoezi haya kwa hisani ya Snacknation Blog