Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Wazo la Biashara Mtandaoni Linaloweza Kukupa Pesa (100%)

Unaweza kutengeneza faida ya hadi TZS 460,000
Wazo la Biashara Mtandaoni Linaloweza Kukupa Pesa (100%) Wazo la Biashara Mtandaoni Linaloweza Kukupa Pesa (100%)

Kwa sasa ni wazi kuwa kila kijana anapenda kumili biashara yake, lakini ni wazi kuwa pamoja na kuwepo kwa taasisi mbalimbali zinazotoa msaada wa kifedha kwa vijana wenye mawazo ya biashara lakini bado mawazo mazuri ya biashara yamekuwa ni magumu na hadimu kupatikana.

Kupitia makala hii ningependa kushiriki na wewe wazo la biashara ambayo unaweza kulitumia kwa asilimia 100 na kuanzisha biashara yako mtandaoni na kuweza kutengeneza pesa kila siku. Kumbuka kwa mujibu wa sheria ni lazima kusajili mawazo yako ya biashara hivyo unaweza kuchukua mawazo haya na kuyasajili na kufanya yako kwa asilimia 100.

Advertisement

Pia ni vyema ufahamu kuwa, mawazo nitakayo ongelea hapa ni mawazo ambayo unaweza kuyafanya kwa muda wowote na pia ni lazima kuwa na mtaji mdogo ili kuweza kufanya mawazo haya kwa asilimia 100, pia kupitia makala hii nitaenda kuonyesha kila kitu ikiwa pamoja na mtaji unao hitaji, pamoja na njia gani za kutumia ili kupata pesa, pamoja sababu nyingine za kwanini mimi binafsi nadhani ni njia bora inayoweza kukupa pesa mtandaoni.

Google Play Store

Kwa kuanza ngoja nikueleze historia kidogo, kwa ufupi kabisa binafsi nimeanza kutengeneza mobile apps tokea mwaka 2014, kipindi hicho kwa hapa Tanzania ilikuwa ni ngumu sana kuweka apps kupitia soko la Play Store. Hii ilikuwa inasababishwa na njia za ulipaji kuwa ngumu kwani ilikuwa ni ngumu sana kufanikisha njia za malipo ili uweze kumiliki akaunti ya Google Play Console kwa ajili ya kuweka app kupitia soko la Play Store.

Sasa hadi leo hii pamoja na kuwepo kwa huduma za M Pesa Mastercard na Airtel Mastercard bado kumekuwa na ugumu kwa baadhi ya watu kulipia dollar $25 ambayo ni sawa na takribani TZS 60,000 kama gharama za kumiliki akaunti ya Google Play kwa ajili ya kuweka app moja tu ambayo mtu huyo hana uhakika kama app hiyo itafanikiwa au lah.

Sasa katika kipindi changu chote cha kutengeneza apps nimekutana na watu wengi sana wakitaka kuweka apps zao kwenye soko la Play Store na wakiwa tayari kulipa kiwango fulani cha pesa, hapa ndio wazo hili lilipo zaliwa… Kwa muda sasa nimekuwa nikiwaza kuwa na huduma ya kusaidia watu kuweka apps kupitia soko la Play Store lakini kwangu binafsi imekuwa ni mtihani mkubwa sana kutokana na muda wangu kuwa mdogo. Ndio maana nimeona leo ni shiriki na nanyi wazo hili kwani sio vyema kubaki na mawazo ambayo watu wengine wangeweza kutumia na kufanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Wazo la Biashara

Sasa wazo lenyewe ni kuwa, unahitaji kusajili akaunti ya Play Store ambayo hiyo akaunti utakuwa unaweka apps za watu mbalimbali kisha watu hao watakuwa wanakulipa wewe kiwango fulani cha pesa kwa kuweka app moja. Kwa mfano unaweza kulipisha angalau Tsh 10,000 kwa app moja na hiyo ni tofauti na huduma ya kutengeneza Icon pamoja na screenshot za App hiyo kama mteja anataka.

Pia unaweza kulipisha Tsh 5,000 kwa kila update ambayo mteja wako atakuwa inafanya kwenye app yake kupitia akaunti yako. Kifupi ni kuwa unaweza kutengeneza angalau TZS 20,000 kwa kila app ambayo inaweka Play Store.

Mtaji

Mtaji unao hitaji hapa ni mdogo sana, hatua ya kwanza unahitaji kuwa na website ya biashara, website itakayo kusaidia pale watu watakapo tafuta kuhusu huduma za kuweka app kupitia soko la Play Store. Mbali na hayo unahitaji akaunti ya Play Store ambayo itasajiliwa kwenye email yako ya pembeni na jina la pembeni. Naposema Pembeni hapa namaanisha tengeneza akaunti mpya ya Google ili kutenganisha kazi na mambo binafsi.

Changamoto

Ukweli ni kwamba hakuna biashara isiyokuwa na changamoto na katika biashara hii pia kuna changamoto zake, moja ya changamoto ambazo pengine ni kubwa kuliko zote ni kuwa Google kwa ujumla haikubali mtindo wa kuwekea watu app Play Store. Sharti ni kwamba ni muhimu kila mtengenezaji wa programu kuwa na akaunti yake ili kuweka app yake kwenye soko la Play Store.

Njia za Kutatua Changamoto Hizo

Moja kati ya njia ambayo unaweza kutumia kuweza kutatua changamoto hiyo kwenye biashara hii ni pamoja kuwa na sheria na vigezo vya app ambazo unazikubali, hakikisha unakubali apps ambazo ni bora na sio app ni app. Hakikisha hizi sheria unaziweka kwenye tovuti yako na mteja hazifahamu kabla ya kutumia huduma zako. Kwa kufanya hivyo utaweza kukwepa kufungiwa akaunti yako kwa kuwekea watu apps kwenye soko la Play Store.

Faida za Biashara Hii

Siku zote kwenye changamoto ndipo biashara ilipo kwa kufanya biashara hii itaweza kupata pesa kwa haraka na kwa urahisi kwani nakuhakikishia wapo watu wengi sana wanao hitaji kupata huduma kama hii, lakini mwisho wa siku biashara ni faida hebu sasa tuangalie faida ya biashara hii kwa muda wa miezi sita tukiwa tunakadiria kuwa unapata wateja watatu kila wiki.

  • Mteja mmoja kuweka App Moja – TZS 10,000
  • Miezi Sita Inakuwa na Wiki – 24
  • Kila wiki Unapata kiasi cha Chini – TZS 30,000
  • Kwa Miezi Sita Utaweza kupata – TZS 720,000
  • Ukitoa Mtaji – TZS 260,000
  • Faida – TZS 460,000

Kama unavyoweza kuona ndani ya miezi sita utaweza kupata faida ya TZS 460,000 kwa kuweka app tu kupitia Play Store. Hapa hatuja jumlisha faida utakazo pata kwenye kutengeneza icon pamoja na screenshot za app mbalimbali. Kitu kingine ni kuwa unaweza kupata wateja zaidi ya hao pale utakapo tangaza biashara yako kupitia sehemu mbalimbali.

Na hilo ndilo wazo la biashara ambalo unaweza kufanya na kuingiza pesa kwa urahisi kupitia mtandao, kumbuka unaweza kupanua zaidi wazo hili kwa kuongeza huduma zaidi pamoja na kupanua zaidi biashara yako ili kusudi uweze kuwapa watu huduma bora zaidi. Kujua zaidi kuhusu biashara mtandaoni soma zaidi hapa.

7 comments
  1. Nimeipenda hii biashara!?ila binafsi nadhani inahitaji taaluma ya it katika kutengeneza hizo apps!nafikiri ni changamoto kubwa kwangu…

  2. Aisee binafsi nimevutiwa na hilo wazo la biashara, na mzidi kubarikiwa sana Tanzania Tech,
    Mi ni mtembeleaji mzuri sana wa Hii site yenu
    Big Up

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use