Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Utaweza kufanikiwa kwa mtaji mdogo kupitia biashara hizi za mtandaoni
Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%) Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Kwa namna yoyote kila mtu anapenda kuwa mjasiri ya mali, lakini ni watu wachache sana wanaofanikiwa kuwa na nafasi hiyo adhimu ya kumiliki biashara ambayo inaweza kukusadia kuingiza kupato cha kutosha.

Kuliona hili leo nimekuleta mawazo ya biashara ambayo natumaini ukiyafanyia kazi utaweza kutengeneza biashara kubwa mtandaoni na hatimaye kufikia ndoto ya kuwa mjasiria amali wa kisasa kabisa hapa nchini Tanzania.

Advertisement

Kumbuka mawazo haya ya biashara hayahiyaji mtaji mkubwa na mtu yoyote kwa wakati wowote anaweza kuanza biashara hizi, kitu cha muhimu ni kuwa na ufanisi na pengine kuwa na nidhamu ya biashara na kuto kukata tamaa.

Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende kwenye mawazo haya ya biashara za mtandaoni ambazo unaweza kuanza kwa mtaji mdogo sana.

Biashara ya Kuuza Saa Mtandaoni

Najua unaweza kuanza kusema “kwani mimi ni mmachinga..” lakini naomba unipe muda wako kidogo nikueleze jinsi ya kufanya biashara hii.

Kupitia kwenye masoko mbalimbali, hasa Aliexpress kunazo smartwatch nzuri sana ambazo unaweza kununua kwa bei nafuu kuanzia dollar 5 hadi 10 na unaweza kuuza hapa Tanzania mara mbili ya kiasi hicho unacho nunulia.

Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Kwa mfano kama unaweza kuona kwenye picha hapo juu, saa hizo zina uwezo wa kupima mapigo ya moyi ikiwa pamoja na uwezo wa kutumika kwenye simu yako ya Android au iOS na ukiangalia thamani yake ni kuanzia TZS 11,600 na kuendelea tena zikiwa na uwezo wa kusafirishwa bure.

Hii inaweza kuwa biashara nzuri sana kwa mtu yoyote mwenye kiasi cha TZS 50,000 na kuendelea, unaweza kufanya biashara hii ya nunua saa hizi na kuziuza kwa urahisi hapa Tanzania.

Saidia Watu Kuuza Bidhaa Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanaujuzi kidogo wa kutumia mitandao ya kijamii basi huenda biashara hii ikawa bora sana kwako.

Kupitia biashara hii utaweza kutengeneza akaunti za mitandao ya kijamii kama Instagram, kisha unaweza kutangaza akaunti yako kwa kiasi cha TZS 50,000 ili iweze kukua haraka alafu kupitia akaunti hiyo unaweka bidhaa za watu mbalimbali ambao wanaziuza.

Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Yaani mtu anapotaka kuuza bidhaa yake anawasiliana na wewe na kisha wewe unaweka picha ya bidhaa kwenye akaunti yako na unaongeza kiasi kidogo cha pesa kwenye bei ya bidhaa uliyopewa na endapo mteja anahitaji bidhaa basi una wasiliana na muuzaji na biashara inapo fanyika basi unapewa asilimia zako unazo ulizo ongeza kwenye bei aliyokuwa nahitaji muuzaji.

Saidia Watu Kusajili Biashara Mtandaoni

Kama unavyojua kwa sasa kila kitu kinaamia mtandaoni, hata usajili wa biashara kwa sasa ni upo mtandaoni. Ukweli ni kwamba kila siku watu hufungua biashara mbalimbali ambazo zinahitaji usajili hata mimi binafsi nilishafikiria kuanzisha biashara hii kutokana na kupata maombi ya kusajilia watu biashara.

Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Kama zilivyo biashara nyingine kwenye list hii, pia biashara hii inahitaji mtaji lakini ni mtaji mdogo sana. Na mtaji huo unaweza kwenda kwenye kujitangaza zaidi hasa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hasa mtandao wa Instagram. Hakikisha unasajili akaunti yenye maneno hayo ya kusajili biashara na pia andika kila kitu unachofanya.

Na hayo ndio mawazo ya biashara ambayo unaweza kuanza kwa mtaji mdogo sana, unaweza kuanza biashara hizi leo kwa kufanya jambo moja baada ya jingine. Unaweza kuanza kwa kufungua akaunti za mitandao ya kijamii kama Instagram na nyingine.

Kama unataka biashara nyingine ambazo zipo tayari kama vile website itakayo kukusaidia kutengeneza pesa mtandaoni kupitia matangazo ya Adsense bila kuandika makala yoyote basi unaweza kupata biashara hizo na nyingine nyingi kupitia hapa.

Mawazo ya Biashara za Mtaji Mdogo Mtandaoni (100%)

Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha kuhusu biashara mtandaoni unaweza kusoma hapa, pia kama unataka kujua hatua za awali za kusajili biashara mtandaoni unaweza kusoma makala hapa na utaweza kusajili biashara yako kwa haraka na urahisi. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use