Hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ilisimekana kuwa kampuni ya Apple imepata hasara kutokana na kushuka kwa mauzo ya simu zake kwa mwaka uliopita, toka mwaka 2018 habari hizi zilipo anza kusamba hakuna ripoti yoyote iliyowahi kutolewa na kampuni ya Apple kuonyesha kukubali kuwa mauzo ya simu za iPhone yameshuka.
Hatimaye hapo jana kampuni ya Apple imeandika barua kwa wawekezaji kuwataka kujua kwamba kweli mauzo ya simu za iPhone kwa mwaka 2018 yalishuka sana. Mbali na hayo barua hiyo ilionyesha kuwa Apple imeshusha kiwango cha matarajio ya mapato kwa robo ya kwanza ya mwaka 2019 kutoka kiasi cha dollar za marekani bilioni $89 na biloni $93 kwa mwaka 2018, hadi kiasi cha dollar za marekani bilioni $84 kwa mwaka huu 2019.
Hata hivyo kupitia barua hiyo Apple imeandika kuwa, tatizo kubwa lilikuwa ni kushuka kwa soko la simu za iPhone nchini china ambapo Apple imedai kuwa ndipo panapo changia mapato kwa kiasi kikubwa. Barua hiyo pia imeainisha kuwa, matoleo mapya ya simu za iPhone hayakupokelewa vizuri kama walivyo kuwa wakitegemea huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni ushindani.
Mbali na hayo Apple pia imetaja sababu nyingine kuwa ni bei ya ubadilishaji battery wa simu hizo kushuka ndio maana watu wengi zaidi walijikita kwenye kubadilisha battery za simu zao zaidi kuliko kununua matoleo mapya ya simu hizo za iPhone.
Tofauti na mauzo ya iPhone, mauzo mangine kwenye bidhaa nyngine za Apple kama vile Apple Watch, Apple Music, Apple iCloud na Apple Computer yameonekana kuongezeka kwa kiasi kikubwa na kuripotiwa kutengeneza zaidi ya dollar za marekani bilioni $10.8 kwa mwaka jana 2018.
Apple imeandika kwenye barua hiyo kuwa, bidhaa kama Apple Watch na AirPods zimeonekana kuongezeka kwenye mauzo kwa hadi asilimia 50 mwaka hadi mwaka, huku ikitaja kuwa bidhaa hizo zimekuwa zikinunuliwa zaidi hasa kwenye kipindi cha sikukuu. Pia Apple imeandika kuwa kompyuta mpya ya Macbook Air iliyozinduliwa mwaka 2018 imeongeza mapato kwa kiasi kikubwa pamoja na iPad Pro mpya za mwaka 2018. Kujua zaidi kuhusu hii unaweza kusoma barua hiyo hapa.
Anyway, kwa upande wangu mimi nadhani ni wazi kuwa mauzo ya simu za iPhone yameshuka sana hasa kutokana na bei ya simu hizo kuwa kubwa. Hii inachangiwa zaidi pale unapongalia simu nyingi nzuri za Android zenye uwezo hata zaidi ya iPhone zilizotoka mwaka 2018 ambazo hupatikana kwa bei nafuu zaidi.
Kwa sasa hapa Tanzania kama unataka simu mpya ya iPhone Max ya laini moja yenye GB 256, unaweza kuipata kuanzia dollar za marekani $1300, ambayo ni sawa na takribani shilingi za Tanzania Tsh 2,990,780. Kama unavyoona bei hii sio rafiki kwa kila mpenzi wa iPhone hivyo nadhani Apple ina kila haja ya kuangalia bei ya bidhaa zake hasa kwenye soko hili la ushindani.