Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Maujanja ya Kufanya Kwenye Picha Zako (Android)

Fanya picha zako ziwe tofauti kwa kutumia njia hizi
Maujanja ya Kufanya Kwenye Picha Zako (Android) Maujanja ya Kufanya Kwenye Picha Zako (Android)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupendelea kuedit picha kwa namna mbalimbali basi ni wazi kuwa lazima umeshajaribu njia mbalimbali kupitia Tanzania tech.

Mbali ya njia hizo bado zipo njia mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kubadilisha picha zako zikawa kwenye muundo wa namna ya kipekee. Kupitia makala hii leo Tanzania tech tumekuletea njia mpya ambazo zinaweza kusaidia kuedit picha zako kwa urahisi na kisasa kabisa.

Advertisement

Najua uko na majukumu mengi hivyo sitapoteza muda wako zaidi na kwa kusema hayo moja kwa moja twende kwenye makala hii.

Badilisha Sura yako Kuwa Katuni

Kupitia hapa Tanzania tech, tumesha ongelea app nyingi sana ambazo zinakusaidia kubadilisha picha kuwa katuni, lakini pamoja na hayo bado zipo app nyingi ambazo unaweza kuzitumia kubadilisha picha zako kuwa katuni.

Kupitia app hii utaweza kubadilisha picha yenye sura yako kuwa katuni kwa asilimia 100, tofauti na app nyingine ambazo hujaribu kubadilisha picha kuwa katuni app hii huweza kufanya hatua hizi kwa asilimia kubwa kuliko app nyingi ambazo umeshwahi kujaribu. Kitu cha msingi jaribu app hii kisha utaniambia… trust me utafurahia sana matokeo.

Download App Hapa

Weka Rangi Kwenye Picha za Zamani

Ni wazi kuwa tunajua kuwa picha za zamani zilikuwa hazi rangi, ndio maana kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuweka rangi kwenye picha za zamani bila kupoteza muda mrefu.

Kama unavyoweza kuona njia hii ni bora na rahisi sana kwa mtu yeyote ambaye ni muhenga na anazo picha za zamani ambazo kwa namna moja ama nyingine hazina rangi na ungependa kuweka rangi kwa kutumia mfumo wa AI basi jaribu app hii kisha utaniambia, trust me utashangazwa na matokeo.

Download App Hapa

Ondoa Background Kwenye Picha Fasta!

Kama unataka kuondoa background kwenye picha kuna njia nyingi hapa Tanzania tech, lakini hadi sasa hakuna njia ya haraka kama hii, kupitia njia hii unachotakiwa kufanya ni kupicha picha na moja kwa moja itaondolewa background na utaweza kuiweka kwenye background nyingine moja kwa moja.

Kama unavyoweza kuona hapo juu, njia hii ni haraka na pia zipo background nyingi mbalimbali ambazo zipo ndani ya app ambazo unaweza kuzitumia kuweka picha yako. Kitu cha muhimu hakikisha unapo piga picha nyuma yako kusiwe na rangi nyingi sana ili kupata matokeo mazuri zaidi, jaribu njia hii kupitia simu yako ya Android kwa kupakua app hapo chini.

Download App Hapa

Kwa leo haya ndio maujanja ambayo na uhakika yatakuacha mdomo wazi, kama unataka kujua zaidi hakikisha unendelea kutembelea Tanzania tech kila siku. Pia unaweza kujaribu njia bora ya kubadilisha picha kuwa video kwa urahisi, kama hadi sasa hujajaribu njia hii basi unapitwa!…

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use