Programu ya VLC ni moja kati ya programu maarufu sana ya kucheza audio pamoja na video, pamoja na kutumiwa na watu wengi sana duniani kote, ni watu wachache sana wanaojua jinsi ya kutumia programu hiyo kikamilifu.
Sasa leo hapa Tanzania Tech tutaenda kufundisha maujanja yote ambayo unaweza kufanya kwa kutumia programu hiyo ya VLC kwa kutumia kompyuta, kumbuka kama unatumia simu hakikisha unasubiria makala yetu inayokuja ambayo tutaenda kuangalia maujanja ya programu hiyo kwa upande wa Simu au Smartphone. Kwa leo, bila kupoteza muda twende tukaangalie maujanja hayo ya VLC kwa upande wa kompyuta.
Tumia Programu ya VLC Kudownload Video YouTube
Kama umekuwa ukitaka kudownload video kupitia youtube bila mafanikio basi usiwe na wasiwasi. Programu ya VLC inakupa uwezo wa kupakua video za Youtube kwa kufauata njia hizi rahisi. Kwa kuanza Ingia Youtube kisha Copy link ya Video unayotaka kudownload
- Fungua programu ya VLC kisha chagua Media > Open Network stream.
- Paste au weka link ya video ambayo ulicopy kutokea YouTube, baada ya hapo bofya kitufe cha Play kilichoko chini kulia.
- Subiri kidogo kisha utaona video hiyo inacheza kupitia programu yako ya VLC, baada ya video hiyo kuanza kucheza nenda juu kabisa alafu bofya Tools > Codec Information hapo utaona box jipya limefunguka. Chini ya hilo box utoana maneno Location kisha Copy link iliyoko kwenye kichumba hicho.
Baada ya ku-copy link hiyo, paste link hiyo kwenye programu yoyote ya kudownload unayotumia, kisha na utaona video hiyo imeanza kudownload, Njia hii ni rahisi zaidi kama unatumia programu kudownload ya IDM.
Tumia Programu ya VLC Ku-Convert Ma-file ya Video
Maujanja mengine ambayo unaweza kufanya kwa kutumia programu ya VLC ni pamoja na kubadilisha Video kuwa audio au kubadilisha video kutoka kwenye mfumo mmoja kwenda mwingine, kwa mfano kutoka MP4 kwenda WMV na nyingine nyingi. Sasa ili uweze kufanya katua hizo unahitaji kufuata hatua hizi.
Tumia Programu ya VLC Kusikiliza Radio za Mtandaoni (Internet Radio)
Maujanja mengine ambayo unaweza kufanya ukiwa na programu ya VLC ni kusikiliza Radio za mtandaoni, Njia hii itakusaidia kuweza kusikiliza Radio za ndani pamoja na za nje ya nchi. Njia hii itawea kufanya kazi endapo utakuwa na Internet kwenye kompyuta yako. Njia za kufuata ni kama zifuatazo.
- Fungua programu ya VLC kisha bofya sehemu ya Playlist, iliyopo kwenye ukingo wa chini kitufe cha tatu kutoka upande wa kulia. Pia unaweza kupata sehemu hiyo kupitia ukingo wa Menu kwa juu bofya sehemu ya View kisha chagua Playlist.
- Baada ya hapo utaona box lingine limefunguka upande wa kushoto hapo shuka chini mpaka sehemu iliyo andikwa Internet, kisha chini yake utaona sehemu mbili moja imeandikwa Jamendo selection na nyingine imeandikwa Icecast Radio Directory bofya hapo na kama una internet kwenye kompyuta yako utaona radio mbalimbali zikionekana, bofya jina la radio mara mbili kusikiliza.
Download Subtitle kwa Kutumia Programu ya VLC
Kama unataka kupakua subtitle ya filamu yoyote, unauwezo wa kufanya hivyo kwa kutumia programu ya VLC. Hatua ni kama zifuatazo.
- Fungua programu ya VLC kisha Play Filamu unayotaka Subtitle yake, baada ya filamu kuanza kucheza bofya sehemu ya View iliyoko juu kabisa, baada ya hapo utaona kibox kipya kimefunguka, chini ya kibox hicho utona neno VLsub bofya hapo
- Baada ya kubofya hapo utaona box jipya limefunguka, Kwenye box hilo hakikisha unachagua lugha unayota pia hakikisha jina la filamu limeandikwa sahihi. Baada ya kuhakikisha yote hayo malizia kwa kubofya Search by name.
- Baada ya hapo utaona subtitle zimetokea ndani ya box hilo kumbuka unatakiwa kuwa na internet kuweza kupakua subtitle. Hakikisha unachagua subtitle unayotaka au inayoendana na jina la filamu yako kisha bofya Download selection na utaona file la subtitle limehifadhiwa mahali filamu ilipo.
Pia kama unataka kutafuta subtitle na unaona programu ya VLC haijapata Subtitle hiyo unaweza kufuata maujanja mengine na kwa njia hizo na ukakika lazima utaweza kupakua subtitle kwaajili ya filamu yoyote unayotaka kuangalia.
Na hayo ndio maujanja niliyo kuandalia kwa siku ya leo, Unaweza kuuliza swali lako kupitia HAPA au kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi kwa vitendo hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.
Naomba kujua jinsi ya kudownload video zenye huwezo wa 1080 youtube