Sababu za Matatizo ya Instagram na Facebook Hapo Jana

Hizi hapa ndio sababu kwanini ulishindwa kutumia Instagram hapo jana
Sababu za Matatizo ya Instagram na Facebook Hapo Jana Sababu za Matatizo ya Instagram na Facebook Hapo Jana

Hapo siku ya Jumatano kuanzia mida ya saa mbili 8:00 PM kwa saa za afrika mashariki mitandao maarufu ya kijamii Instagram, Facebook na Facebook Messenger ilikuwa haipatikani hewani kutokana na mitandao hiyo kupitia hatua za marekebisho yaliyofanya baadhi ya watu kushindwa kabisa kutumia mitandao hiyo.

Kwa hapa Tanzania, hali hii pia ilikwepo kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo, huku watumiaji wengi wakiwa wanashindwa kuingia kwenye akaunti zao na wengine wakishindwa kupost post mpya.

Advertisement

Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, inasemekana kuwa tatizo hilo la lilisababishwa na mtandao wa Facebook kufanya maboresho ya tovuti zake hasa kwenye upande wa data kazi (Data base) ambayo hii ndio husaidia watu kuhifadhi data za watumiaji pamoja na kuruhusu watumiaji kuingia kwenye akaunti zao na kupost na kufanya vitu vingine mbalimbali.

Kwa mujibu wa Forbes, Facebook ilitumia ujumbe kwenye baadhi ya akaunti, ujumbe uliokuwa ukiwataka watumiaji kujua kuwa mtandao huo unafanya marekebisho ya data kazi na kuna uwezekano wa mtumiaji kushindwa kutumia akaunti yake kwa muda huo ambapo mtandao huo utakuwa unafanyiwa marekebisho hayo.

Sababu za Matatizo ya Instagram na Facebook Hapo Jana

Hata hivyo kwenye maelezo zaidi ya kwenye ukurasa huo, yalisema kuwa inawezekana wewe ukaona huwezi kutumia mitandao hiyo lakini mwenzako akaweza kutumia mitandao hiyo. Kwa mfano sisi Tanzania tech, kwa upande wetu tulichelewa sana kupata taarifa hii kutokana na tatizo hili kutokwepo kwenye akaunti yetu ya Facebook wala Instagram, na baadae sana tatizo hili ndipo lilianza kuonekana kwa baadhi ya nyakati.

Hadi sasa Facebook imesha tatua tatizo hilo na mitandao hiyo kwa sasa imerudi hewani na unaweza kuitumia kama kawaida. Hata hivyo Facebook imekanusha kuwa mitandao hiyo ilishindwa kuwa hewani kutokana na kuzidiwa au shambulizi la DDOS.

Instagram na Facebook ni moja kati ya mitandao mikubwa duniani, huku ikiwa na idadi kubwa ya watu wanaotembelea mitandao hiyo kwa pamoja hivyo kukosekana kwa mitandao hii lazima kumesababisha hasara hasa kwa watumiaji wa huduma hizo hasa wanaotumia matangazo ya mitandao hiyo kuwafikiwa wateja mbalimbali.

Hadi sasa Facebook bado haijatoa maelezo mengine ya nini kilicho sababisha matatizo hayo, na itakuwaje kwa wale wanaofanya matangazo kwenye mitandao hiyo. Hadi hapo tutakapo pata taarifa kamili kutoka kwa msemaji wa mitandao hiyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha zaidi.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mitandao ya Facebook na Instagram kushindwa kuwa hewani kwa muda, siku za karibuni mtandao wa Facebook ulishindwa kuwa hewani kwa baadhi ya nchi na baada kurudi kufanya kazi bila baadhi ya watu kwenye nchi nyingine kujua.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use