Waziri wa mambo ya ndani hapa Nchini Tanzania Mwigulu Nchemba amesema kuwa amepata malalamiko ya baadhi ya watu mtandaoni kutumia jina lake kufanya utapeli.
Akiongea na waandishi wa habari Mwigulu Nchemba amesema “Nimepata malalamiko kuwa watu wamesajili hadi kwa jina langu na wanajitambulisha kuwa ni waziri wa mambo ya ndani, hivyo basi niwaombe watumishi kuacha kufanyia kazi maagizo yoyote ambayo yanatolewa na watu hao kwa njia ya simu na kujikuta wanatapeliwa fedha, ” imeandikwa na gazeti la nipashe.
Hata hivyo Waziri huyo alitoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo ya kitapeli na kuwa baadhi ya watu wanaojihusisha na utapeli huo kutumia majina ya viongozi kusajilia simu zao ili kuwatishia watumishi.
Mwigulu aliwataka watu hao kuacha tabia hiyo mara moja kwani pale watakapo bainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na watu wanao sajili line kwa majina ambayo sio ya kwao.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : Nipashe