Wakati zikiwa zimebaki siku kadhaa hadi kuzinduliwa kwa simu mpya ya Galaxy Note 9, Kampuni ya Samsung imeanza kuonyesha matangazo tofauti kwaajili ya simu hiyo. Siku ya leo Samsung imetoa matangazo matatu, huku kila tangazo likionyesha maboresho yanayo tarajiwa kuja kwenye simu hiyo.
Tangazo la kwanza linaonyesha kuwa simu hiyo itakuja na bettery kubwa, na kwa mujibu wa mitandao mbalimbali simu hiyo inasemekana kuja na battery yenye ukubwa wa 4000mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu zaidi.
Tangazo lingine linahusu uwezo wa simu hiyo, ambapo inasemekana simu hiyo ya Galaxy Note 9 itakuja na processor yenye nguvu, huku ikisemekana Note 9 itakuja ikiwa inatumia processor za Exynos 9810 au Snapdragon 845.
Tangazo la mwisho linahusu ukubwa wa ndani wa simu hiyo, ambayo mwanzo kulikuwa na tetesi kuwa simu hiyo itakuja na toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 512 hivyo kukupa uwezo wa kutumia simu hiyo bila kuwa na wasiwasi kuhusu kujaa kwa haraka kwa simu hiyo.
Matangazo haya yote yanahashiria simu ya Galaxy Note 9 sasa ipo tayari na imebaki tu kuzindua simu hiyo hapo siku ya alhamisi ya tarehe 9 ya mwezi wa nane mwaka 2018.