Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Hizi hapa app ambazo unaweza kutumia kupakua apps nyingine kwa urahis na haraka
Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Ukweli ni kwamba kuna watu wengi sana wanaotumia simu za Android ambazo hazina uwezo wa kupakua programu kutoka soko la play store. Hii inafanya watu wengi kushindwa kupakua kwa haraka programu za muhimu au kukosa update za programu hizo kwa wakati.

Kuliona hili leo nimekuletea list ya masoko ya apps ambayo yatakusaidia kupakua apps za Android kwa urahisi, ikiwa pamoja na kupata update za apps mbalimbali kwa urahisi na haraka.

Advertisement

Kumbuka kuwa, Google hairuhusu mbunifu yoyote kuweka apps ambazo uruhusu watu kupakua apps nyingine ndani yake hivyo, app zote ambazo zipo kwenye list hii hazipatikani kwenye soko la Play Store na badala yake utaweza kupakua kupitia link maalum hapo chini.

Aurora Store

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Aurora Store ni moja kati ya app ambayo inakupa uwezo wa kupakua app mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii inatumia mfumo kama wa Google hivyo kuna wakati unahitaji akaunti ili kuweza kupakua baadhi ya App. Lakini kifupo app hii ni nzuri sana na naweza kusema huu ni mbadala mzuri sana wa app ya Play Store kwa wale ambao simu zao hazina app hiyo.

Download App Hapa

Appvn

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Appvn ni app nyingine ambayo itakusaidia kupakua app nyingi kwa urahisi na haraka, tofauti ya app hii na nyingine ni kuwa kupitia soko la Appvn utaweza kupakua app ambazo zinauzwa kwenye soko la Play Store lakini hapa utazipata bure kabisa. Unaweza kujaribu soko hili kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Aptoide

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Aptoide ni app nyingine ambayo itakusaidia kupata app mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii ni kama app ya kwanza kwenye list hii na utaweza kupakua app zote ambazo zipo kwenye soko la Play Store na utaweza kupakua kwa app zote kwa kutumia app hii.

Download App Hapa

AC Market

Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

AC Market ni app nyingine ambayo itakusaidia kupakua app nyingine kwa urahis na haraka. App hii pia ni kama soko la Play Store na app zote ambazo ziko kwenye soko la Play Store utaweza kuzipata hapa kwenye soko la AC Market. Unaweza kujaribu soko hili kwa kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Na hiyo ndio list ya apps ambazo ni mbadala wa soko la Play Store, Kama unataka kujua app nyingine nzuri zaidi ambazo zinaweza kukusaidia kupakua audio na video kwa urahisi na haraka unaweza kusoma hapa, utaweza kupata nyimbo zote mpya kwa urahisi na haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use