Wakati bei ya hisa za Facebook ikiendelea kupanda chati kila siku, Mkurugenzi mtendaji na mwanzishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg, sasa amempita Warren Buffett kwa kuwa mtu tajiri zaidi wa tatu duniani.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya Bloomberg, utajiri wa Mark Zuckerberg sasa unakadiriwa kuwa ni dollar za marekani bilioni $81.6 sawa na Shilingi za Tanzania Trilioni 185.5, Mark Zuckerberg sasa yuko chini ya mgunduzi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates ambaye anao utajiri wa dollar za marekani Bilioni 94.2, huku akifuatiwa na tajiri wa kwanza wa dunia kwa sasa ambaye ni mgunduzi wa mtandao wa Amazon, Jeff Bezos ambaye yeye anao utajiri wa dollar za marekani bilioni $142.
Hata hivyo japokuwa Facebook imeendelea kupata vikwanzo mbalimbali kutoka kwa mashirika na serikali za nchi mbalimbali, bado hisa za kampuni hiyo zimeonekana kupanda kwa kasi huku siku ya ijumaa kukiwa na ongezeko la asilimia 2.4% ambapo bei ya hisa ya kampuni hiyo ikiwa inanzia dollar za marekani $203 sawa na Tsh 462,000.
Tumesikia mara nyingi kupanda na kushuka kwa hisa za makampuni haya ya teknolojia kukifanya wagunduzi wake kupanda au kushuka kwa utajiri wao, hivyo inawezekana kabisa Warren Buffett akarudi kwenye nafasi yake siku za karibuni kwani hata hivyo wamepishana na Mark Zuckerberg kwa tofauti ndogo. Warren Buffett kwa sasa anao utajiri wa dollar za marekani Bilioni 81.2.
Duh, jamaa anazindu kuwa tajiri tu mh.