Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kujua Mara Ngapi Unafungua Simu Yako kwa Siku

Utaweza kujua kama unatumia simu yako kupita kiasi
Jinsi ya Kujua Mara Ngapi Unafungua Simu Yako kwa Siku Jinsi ya Kujua Mara Ngapi Unafungua Simu Yako kwa Siku

Kama unavyojua kila kitu ukizidisha ni tatizo, hata utumiaji wa smartphone uliopitiliza ni tatizo kubwa sana ambalo watu wengi hasa vijana wanalo lakini hawajui au wanachukulia poa kwa sababu wanaona kama sio tatizo kubwa.

Kifupi ni kuwa, uraibu wa smartphone ni ugonjwa kama magonjwa mengine ya uraibu ambayo mara nyingi yanahitaji kutibiwa kisaikolojia. Sasa kwa kuwa mimi sio mwana saikolojia leo nitakusaidia kwa upande wa teknolojia jinsi ya kutumia teknolojia ili kujua kama unalo tatizo la uraibu au kupenda smartphone kupita kiasi.

Advertisement

Pamoja na kujua dalili za ugonjwa wa kupenda smartphone kupita kiasi, sasa leo ngoja nikuongezee hii ambayo inaweza kusaidia sana. Hivi ulisha wahi kujiuliza unafungua simu yako mara ngapi kwa siku, yani ni mara ngapi una unlock simu yako ili kutumia..? Sasa najua ni ngumu kuhesabu hivyo nitaenda kukuonyesha njia ya kuhesabu ili kujua kama una tatizo hili la uraibu wa smartphone.

Kutana na Unlock Clock, hii ni app mpya ya Google ambayo inakusaidia kuhesabu mara ngapi unafungua simu yako, uzuri wa app hii ni kuwa haipo kama app nyingine bali hii inakuwa kama wallpaper ya saa kwenye simu yako na kila unapofungua simu yako moja kwa moja huesabu na saa hiyo kubadilka juu ya kioo chako ili kuonyesha mara ngapi umefungua simu yako, yani kama hivi..

Sasa kama unavyoweza kuona njia hii inaweza kukusaidia sana kujua ni mara ngapi unafungua simu yako, hii ni nzuri kwani kama utapata namba kubwa sana mwisho wa siku basi utajua kweli unatumia simu yako kupitiliza kwani kuna watu wengi wanafungua simu zao bila hata kuwa na mahitaji ya muhimu ya kutumia. Unaweza kupakua app hiyo kupitia hapo chini.

Na uhakika utakapo tumia app hii basi utaweza kujua moja ya dalili ambayo inaweza kuashiria kama unao ugonjwa wa kupenda smartphone kupita kiasi. Kumbuka hii ni moja tu ya njia ya kutambua kama unao ugonjwa huo, kama unataka kujua zaidi hakikisha unasoma makala yetu yenye kuonyesha dalili za kupenda smartphone kupita kiasi.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unasoma hapa ili kujua jinsi unavyoweza kupokea au kukata simu bila kuishika kupitia simu yako ya Android. Kama unataka kujifunza maujanja zaidi hakikisha una subscribe kwenye channel yetu hapa ili kujifunza zaidi kwa vitendo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use