Kwa mara ya kwanza kabisa tangu kampuni ya Google ilipo nunua mtandao wa YouTube mwaka 2006 ikiwa ni zaidi ya miaka 14 iliyopita, hivi leo kampuni hiyo kwa mara ya kwanza imetengeza mapato ya mtandao wa YouTube kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita yaani January 2019 hadi December 2019.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kutoka kampuni mama ya Google yani Alphabet. YouTube inaingiza takribani billion $5 tano za marekani kwa muda wa miezi mitatu ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania trilioni 11.5 kwa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo.
Mbali na hayo, kwa mujibu wa ripoti hiyo YouTube imeingiza zaidi ya bilioni 15 za marekani kwa mwaka mzima ambayo ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote ya kampuni ya Google. Mbali na hayo YouTube imeingiza mapato ya ziada ambayo ni zaidi ya dollar za marekani bilioni $5.3, kutoka kwenye mapato ya ziada kutoka kwenye biashara yake ya YouTube Premium ad-free na YouTube Music Premium.
Kwa jumla, Alfabeti imeingiza mapato ya dola bilioni 46 kwa robo iliyomalizika Desemba 31, 2019, ikiwa ni tofauti ya asilimia 17 ikipanda zaidi ya mwaka 2018. Ambapo kampuni hiyo mama ya Google ilikuwa na mapato ya dola bilioni 10.7 ambayo ilikuwa ni faida ya mwaka huo.
Kampuni hiyo inasema, Biashara ya utafutaji ya Google (Google Search) inabaki kuwa chanzo namba moja cha mapato kwa kuingiza kiasi cha dola bilioni 27.2 kwa robo hiyo.
Lakini kando na mapato ya matangazo ya YouTube, Google pia imetangaza mapato ya kifedha ya tawi lake la kompyuta wingu (Cloud Computing). Ambapo ripoti hiyo imesema Google Cloud ilitengeneza dola bilioni 2.6 katika mapato kwa robo hiyo ya mwisho ya mwaka 2019.
Kama unataka kujua ripoti kamili ya mapato hayo ya kampuni ya Google na YouTube kwa ujumla unaweza kusoma ripoti kamili ya mapato hayo kupitia tovuti ya Alphabet hapa.