Hapo jana kampuni ya Samsung imezindua simu mpya za Samsung Galaxy S21, kama ilivyo tarajiwa simu zote zimekuja na sifa ambazo watu wengi tulikua tunakujua kutokana na tetesi mbalimbali mtandaoni.
Lakini pamoja na kujua sifa na bei ya simu hizi kuna baadhi ya mambo ambayo nadhani watu wengi huwenda wakawa hawajui na kupitia makala hii ningependa ujue kabla ya kununua simu hizi mpya.
Nitajitahidi kuandika maneno machache ili uweze kuelewa na usichoke kusoma kwani najua maneno mengi yanachosha sana. Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi, twende kwenye makala hii moja kwa moja.
TABLE OF CONTENTS
Bei ya Galaxy S21 ni Ndogo Kuliko Galaxy S20
Wakati simu za Samsung Galaxy S21 na simu nyingine zikiwa na maboresho kuliko simu za mwaka jana za Galaxy S20, usishangae pale unapo enda kununua simu hizi na kukuta Galaxy S20 ikiwa inauzwa kwa bei ghali kuliko Galaxy S21.
Kwa mfano kwa sasa, Galaxy S21 inauzwa kwa takribani shilingi za Kitanzania TZS 1,870,000, wakati galaxy S20 inauzwa kwa takribani TZS 2,300,000. Unaweza kuona utofauti mkubwa sana. Kujua zaidi kwanini kuna utofauti huu endelea kusoma makala hii.
Galaxy S21 Imetengezwa kwa Plastic
Wakati matoleo mengine ya Galaxy S21 Plus na Galaxy S21 Ultra yakiwa yametengezwa kwa aluminium Frame na Glass, Galaxy S21 imetengezwa kwa makava ya palstiki kwa nyuma pamoja na frame au utepe wa aluminium.
Tofauti na matoleo ya Galaxy S20 ambayo yote yalikuwa ni matoleo yaliyo tengenezwa kwa Glass pamoja na frame au utepe wa aluminium, pengine hii ni moja ya sababu kwanini toleo la Galaxy S21 ni toleo la bei rahisi kuliko Galaxy S20.
Galaxy S21 Hazina Sehemu ya Memory Card
Wakati toleo la mwaka jana la Galaxy S20 likiwa na sehemu ya memory card yenye uwezo wa kutumia memory card yenye uwezo wa hadi TB 1, matoleo mapya ya simu za Samsung Galaxy S21 yote hayana sehemu ya kuchomeka memory card.
Samsung imekuwekea ukomo na utaweza kuchagua simu yenye uwezo wa kati ya GB 128, GB 256 au GB 512. Kumbuka bei inaongezeka kila unapofikiria kuwa na simu hii yenye uhifadhi mkubwa zaidi.
Galaxy S21 Ina Resolution Ndogo Kuliko S20
Simu ya Galaxy S21 inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.2, japokuwa kioo hichi ni sawa kabisa na kioo cha Galaxy S20, lakini moja kati ya kitu kimepunguzwa kwenye kioo cha Galaxy S21 ni pamoja na uwezo wa resolution.
Galaxy S20 inakuja na resulution ya hadi pixel 1440 kwa 3200, kwa upande mwingine Galaxy S21 inakuja na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400. Japokuwa watumiaji wengi wa kawaida wanaweza wasione tofauti lakini kifupi hii ni tofauti kubwa sana.
Hakuna Chaja kwenye Box la Galaxy S21
Kwa kuwa kampuni ya Apple imekuwa na mtindo wa kuanzisha tamaduni nyingi sana, hatimaye sasa tamaduni mpya inabidi uzoee ni kwa simu nyingi kuanza kuja bila chaja kwenye box. Simu zote za Galaxy S21 zitakuja zikiwa hazina chaja kwenye box.
Badala yake, simu hizo zitakuja na waya wa USB C pekee ndani ya box, na kama utakuwa unataka chaja au (Charge Brick) basi unaweza kununua kwa takribani TZS 15,000 hadi TZS 25,000 kulingana na chaja.
Galaxy S21 Ultra Kuja na Kalamu Maalum
Mwaka huu Galaxy S21 Ultra ndio simu yenye sifa nyingi na bora zaidi, kwa mfano simu hii inakuja kwa machaguo matatu ya ROM yani GB 128, GB 256 na GB 512. Pia mbali ya hayo utaweza kuchagua kati ya GB 12 au GB 16 za RAM.
Mbali na hayo Galaxy S21 Ultra inakuja na kalamu maalum ambayo kalamu hii haina sehemu ya kuweka kalamu hiyo kama ambavyo inakuwa kwenye simu za Galaxy Note. Lakini unaweza kununua kava ambalo unaweza kunatisha simu hii kwa pembeni
Mbali na hayo kalamu hiyo haina sifa yoyote ya muhimu kwani haina bluetooth na haina sifa nyingine yoyote, lakini unaweza kununua kalama ya bluetooth yenye sifa zaidi na uwezo zaidi.
Kwa sasa hayo ndio mambo ambayo nimeona kuhusu simu hizi mpya za Samsung Galaxy S21, kama unataka kujua sifa kamili za simu hizi unaweza kusoma hapo chini.
- Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S21 5G
- Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S21 Plus
- Sifa na Bei ya Samsung Galaxy S21 Ultra
Kama unataka kujua zaidi unaweza kulinganisha simu hizi mbili kupitia tovuti ya price in tanzania, pia unaweza kusoma sifa na bei ya simu nyingine kupiti tovuti hiyo hiyo.
Kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung basi unaweza kusoma hapa kujua list ya simu za bei rahisi za Samsung unaweza kununua kwa sasa, pia utaweza kujua sifa kamili za simu hizo.