Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo ya Muhimu ya Kuyajua Kuhusu Mtandao wa Facebook

Hii ndio historia fupi ya facebook na mambo mengine usiyoyajua
Facebook Jewajua Facebook Jewajua

Wote tunaujua mtandao wa facebook na wengi wetu tunazo akaunti zaidi ya moja kwenye mtandao huo, lakini na uhakika mambo haya ulikua huyajui. Basi kama kawaida ya kila jumapili tuko hapa kukujuza mambo kama haya ambayo ulikua uyajui… let’s goo!

  • Mara ya Kwanza Facebook Ilikuwa Inaitwa Facemash

Mwanzoni mgunduzi wa facebook Mark Zuckerberg akiwa mwaka wa pili wa chuo alitengeneza tovuti aliyo ipa jina la Facemash, tovuti hii ambayo baadae ndio ilikuwa facebook ilikuwa maalum kwaajili ya wanafunzi wa chuo cha Harvard ambapo ilikua ikiruhusu wanafunzi kulinganisha picha za wanafunzi wa wawili na kuchagua yupi anae vutia zaidi.

Advertisement

  • Mwanzo Facebook ilikuwa na Jina la TheFacebook

Baada ya Facemash Facebook baadae ilibadilika tena na sasa ilitwa thefacebook ambapo mwaka 2005 ilibadilika tena na kuwa Facebook pekee.

  • Unaweza Kuingia kwenye Tovuti ya Facebook kwa Haraka Hivi..

Faceboo inayo njia nyingi sana za kuingia kwenye tovuti yake lakini njia rahisi sana kama unataka kuingia kwenye tovuti ya facebook kwenye kompyuta basi rahisi kabisa unaweza kuandika fb.com

  • Facebook Inakulipa Pesa Ukiweza Kudukua Tovuti au App Yake

Kama wewe ni mtaalamu wa mtandao na unaweza kufanya udukuzi, basi ni vyema kuweka nguvu zako kwenye vituvya msingi kama kudukuwa tovuti au app ya facebook kwani facebook itakulipa pasa ukiweza kufanya hivyo. Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali facebook inaweza kulipa kuanzia dollar $500 sawa na Tsh 1,119,700.00 hadi dollar $10,000 sawa na Tsh 22,394,000.00 hii ni kutokana na aina ya udukuaji, sababu za kulipa ni kuwa unawasaidia kujua mapungufu ya tovuti yao kwa haraka hivyo get busy anza kudukua sasa..

  • Ukurasa Wenye Like Nyingi Kwenye Facebook

Ukurasa wenye like nyingi facebook ni ukurasa unaoitwa Facebook for Every Phone ukurasa huo una like zaidi ya 495,624,193 na ndio ukurasa wenye like nyingi ukifuatiwa na ukurasa wa Facebook yenyewe wenye like zaidi ya 190,220,342 na nafasi ya tatu ikiwa kwenye ukurasa wa Youtube wenye Like zaidi ya 82,928,416.

Na hayo ndio ndio baadhi ya mambo machache ambayo nimekuandalia jumapili ya leo kuhusu Facebook, kamauna jambo la kuongeza usiache kutuambia kwenye sehemu ya maoni hapo chini nasi tutaongeza makala hii moja kwa moja.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Wikipedia, LEMMiNO

6 comments
  1. Msaada jamani nahitaji kuanzisha mtandao wa kijamii kama insta, fb, n.k naomba ushauri watu gan wateweza kunitengenezea applicatin yangu?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use