Mambo Muhimu ya Kujua Kabla ya Kununua Kompyuta Iliyotumika (Used)

Kama unataka kununua Kompyuta iliyotumika basi haya ni baadhi Mambo muhimu ya kuzingatia
kompyuta iliyotumika kompyuta iliyotumika

Linapokuja swala la kununua kompyuta iliyotumika ni dhahiri sana lazima panaitajika umakini wa hali ya juu, siku hizi kumekuja mitandao ambayo unaweza kununua vitu hivi bila hata ya kumjua mtu anae kuuzia. Hii inaongeza wasiwasi kwa mnunuzi kutokana na kwamba unakuta humjui mtu anae kuuzia Tofauti na hapo awali watu walikua wanauziana bidhaa wanaojuana tu.

Kama ulisha wahi kununua bidhaa iliyotumiaka lazima utakua unajua kuwa usipokua makini unaweza kununua bidhaa ambayo haifai kwa matumizi mengine, hivyo leo Tanzania tech tunakusaidia katika hilo kwa kukuletea mambo muhimu ya kuzingatia wakati unanua kompyuta iliyotumia. Mambo haya ni muhimu sana kuyangali na unapoweza kufanya hivyo basi utaweza kusogeza karibu uwezekano wa kupata kompyuta inayofaa kwa matumizi yako ya baadae.

Advertisement

  • Kujua Kompyuta Unayotaka

Kabla ya kununua kompyuta ya aina yoyote ni lazima ujue kwanza ni kompyuta gani unataka na kwa matumizi gani, hii ni muhimu sana kuliko kitu chochote kwani watu hua wanajua wanataka kompyuta tu lakini hawajui wanataka kompyuta ya matumizi gani. Kwa kujua kompyuta unayotaka itakusaidia kujua sifa za kompyuta unayotaka hivyo itakusaidia kurahisisha zoezi zima la kutafuta kompyuta unayotaka.

  • Angalia Kampuni Iliyo Tengeneza Kompyuta Hiyo 

Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya makampuni ambayo hayako vizuri sana katika utengenezaji wa kompyuta hivyo ni vyema kuangalia sana unapotaka kununua kompyuta iliyotumika. Ni vizuri kuwa makini sana na kompyuta ambazo zina majina ambayo hayajulikani sana kwani hata upatikanaji wa vifaa vya kompyuta hizo hua ni mgumu sana hivyo ni vyema kuchagua majina ya kompyuta ambazo zinajulikana kwa kiasi flani, hii itakusaidia kupata vifaa vya kompyuta yako hiyo pale inapo haribika.

  • Angalia Kompyuta hiyo ni ya Mwaka Gani

Jambo lingine ambalo litakurahisishia kupata kompyuta bora ni kuangalia mwaka wa kompyuta hiyo, yaani hapa inamaana mwaka wa kompyuta hiyo kutengenezwa kwani kompyuta nyingi ambazo zinakuwa ni za miaka ya zamani mara nyingi zinakuwa hazina ubora unaotakiwa na ukiangalia kwa makini sana unaweza kukuta kompyuta hiyo inao ubovu flani hivyo ni vyema kuwa makini sana na hilo. Unaweza kununua kompyuta za kuanzia mwaka 2010 na kuendelea kwani hizi angalau huwa zinakuwa na ubora flani, Pia unaweza kutizama mwaka wa kompyuta kwa kuangalia nyuma ya kompyuta au unaweza kutumia (Google) kwa kutafuta jina na model ya kompyuta yako.

  • Angalia Kompyuta hiyo Imetumika kwa Muda Gani 

Ni vizuri na ni jambo la msingi kujua kompyuta unayotaka kununua imetumika kwa muda gani kwani kwa kujua hilo utapata makadirio ya uzima wa kompyuta hiyo, kwa mfano kompyuta iliyotumiaka miaka mitano au kumi uwezekano wa kompyuta hii kuendelea kutumika ni mdogo sana hivyo ni vyema kuangalia hilo. Unaweza kuangalia hili kwa kumuuliza muuzaji kama ni mwaminifu au unaweza kumuuliza kama alinunua kompyuta hiyo ikiwa mpya na kama alinunua ikiwa mpya basi angalia mwaka wa kompyuta hiyo kutengenezwa na hapo utaona kompyuta hiyo imekaa muda gani.

  • Angalia kwa Makini Kama Kompyuta Hiyo Imefunguliwa

Kama kompyuta hiyo ni laptop ni vyema kuangalia kama imefunguliwa  kwani mara nyingi kompyuta nyingi ambazo zimefunguliwa hua na matatizo mengine madogo madogo pia kumbuka kuangalia pembeni kwenye kava la kompyuta hiyo kama kuna michubuko inayosababishwa na ufunguaji holela wa kompyuta hiyo.

  • Angalia Vifaa vya Nje (Hardware) vya Kompyuta Hiyo 

Kuangalia vifaa vya nje ni kitu cha msingi sana inapokuja katika swala la kununua kompyuta iliyotumika, unaweza kuangalia haya yote kwa hatua, kwa mfano unaweza kuanza kwa kuangalia battery, alafu uka angalia kioo cha kompyuta hiyo kisha ukaangalia sehemu za kuweka flash na sehemu nyingine kama hizo kisha ukamalizia na keyboard na Mouse hili ni la muhimu sana kukumbuka kwani watu wengi huangalia mouse lakini wanasahau kuangalia keyboard hivyo ujikuta wamenunua kompyuta ambayo kuna baadhi ya vibonyezo kwenye keyboard havifanyi kazi kabisa hivyo ni vyema kuwa makini.

  • Angalia Vifaa vya Ndani vya Kompyuta Hiyo

Kwa kuangalia vifaa vya ndani ikiwa pamoja na sifa za kompyuta hiyo utaweza kukamilisha na kujua kama kompyuta hiyo ni nzima na inafaa wewe kununua. Unaweza kufanya hivyo kwa kuanza kuangalia RAM kisha Hard Drive pamoja na Bios kama haina Password ikiwa pamoja na Motherboard ya Kompyuta yako.

Basi kwa kufanya hayo yote hapo juu utakuwa umefanikiwa kuangalia na kujua yote ya muhimu pale unapotaka kununua kompyuta iliyotumika, kama bado kuna jambo ambalo unahisi nimesahau basi usisite kutuandikia maoni yako hapo chini na tuna ahidi ku-update makala hii pale tutakapo pata mambo mengine ya muhimu.

Ili kupata habari zote za Teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

4 comments
  1. Sina mengi yakusema zaidi ya kuwapongeza kwa kazi nzuri.

    ushauri

    watanzania wengi hawajaweza kupata blog hii au app
    naomba mfanya adversrmnt nyingi ili watu waweze kuipata .
    mchango wangu nita share zaidi
    Ahsanteni

  2. nimependa hii hakika hata madalali wamtaani waki tembelea blog yenu wanaweza kuepukana namtatizo yakurudishiwa bidha kwa watejawao nakuwaondolea baadhi ya vikwazo kamahivyo katika kazizao

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use