Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo Matano 5 Muhimu Kujua Kuhusu Kampuni ya Apple

Inawezekana ulikua hujui haya kuhusu kampuni ya Apple
apple Inc apple Inc

Wote tunaijua kampuni ya Apple, kampuni ambayo inaongoza kwa kutengeneza simu za iphone ambazo pengine nje ya Tanzania ni simu ambazo zinaongoza kwa kutumiwa na watu wengi zaidi, lakini leo hatuta ongelea kuhusu hilo bali leo nataka nikujuze kidogo kuhusu kampuni ya Apple.

  • Ronald Wayne alikua Mgunduzi wa Apple

Apple Computer ilianzishwa mwaka 1976 na ilianzishwa na watu watatu yaani Ronald Wayne, Steve Wozniak pamoja na Steve Jobs, lakini baada ya wiki mbili tu za kampuni hiyo Ronald Wayne aliamua kuuza share yake ambayo ilikua asilimia 10 kwa kiasi cha dollar za marekani $800..duh jamaa huyu hakuwa na uvumilivu kabisa..kwani angelikuwa na asilimia hizo 10 za hisa mpaka sasa hisa hizo zingekuwa na thamani ya bilioni 60 za marekani.

Advertisement

  • Steve Jobs aliacha Kazi Apple

Tarehe 16 mwezi wa tisa Mwaka 1985 mmoja wa wagunduzi wa Apple Steve Jobs aliacha kazi rasmi na kujiuzulu kutoka kwenye kampuni aliyoigundua yeye na wenzake, hii ni baada ya ushindani wa kitawala ulio tokea kati yake yeye na John Sculley mmoja wa watu ambao steve aliwaleta kwenye kampuni hiyo kutoka kampuni ya Pepsi-Cola. Jamaa huyo alifanya kazi na Steve kama viongozi na baadae wawili hao walitofautiana na ndipo kamati kuu ili amua kuingilia kati na kumchagua John Sculley kama mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo.

Kitendo hicho kilimchukiza steve na ndipo alipo amua kuacha kazi rasmi kampuni ya Apple na kwenda kuazisha kampuni yake nyingine iliyoitwa Next. Kampuni hii  ilikua inafanya kazi ya kutengeneza programu mbalimbali pamoja na kompyuta, Mwaka 1996 kutokana na kutetereka kwa kampuni ya Apple baada ya Steve Jobs kuondoka, Apple ili nunua kampuni ya Next na kama sehemu ya makubaliano ya ununuzi huo Steve Jobs alirudi kuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Apple.

  • Vipeperushi Vingi vya Vifaa vya Apple Vina onyesha Saa 9:41

Hivi ulisha wahi kujiuliza kwanini karibia kila kipeperushi cha kifaa kutoka kampuni ya Apple kina onyesha Saa 9:41.?, Kama ulikua hujui basi hii ndio sababu, Mwaka 2007 tarehe 9 January saa 9:41 asubuhi Steve Jobs alitangaza iPhone kwa mara ya kwanza kabisa. Now you know..!

  • Apple Ilisha Wahi Kutengeneza Video Game

Kama wewe ni mpenzi wa video game lazima utakua unajiuliza kwanini kampuni kubwa kama Apple haina Video Game kama vile ilivyo PS4 kwa Sony au XBOX kwa Microsoft..?. Lakini kama ulikuwa hujui hapo zamani za kale.. Mwaka 1995 kampuni ya Apple ilisha wahi kutengeneza Video Game iliyo-kuwa inaitwa Apple Pippin, kifaa hicho hakiku fanya vizuri kabisa na kili kufa mapema tu baada ya kuzinduliwa kwake, mbaya zaidi Apple kupitia kifaa hicho ili uza nakala 42,000 tu! duniani kote na kilikua na game 18 pekee…Mhh hapa kweli Apple ilichemka.!

  • Maneno Yote Unayo Sema na Programu ya SIRI yana hifadhiwa na Apple 

Kama wewe ni mtumiaji wa bidhaa za Apple, hapa namaanisha iPhone basi lazima utakuwa unaijua programu ya SIRI, programu hii inakusadia kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako ya iPhone kwa kutumia maneno, kitu cha muhimu kujua ni kuwa kila neno unalo-ongea na programu hiyo lina sikilizwa na kuhifadhiwa na Apple kwa muda wa miwili. Hivyo basi kumbuka kila unapo ongea na programu hiyo jua kuna mtu kazi yake kusikiliza na kuifadhi sauti yako kwa muda wa miaka miwili. Sehemu hii imeandikwa kwenye sehemu ya ukurasa wa vigezo na masharti unapo anza kutumia programu hiyo ya SIRI kwa mara ya kwanza.

Na hayo ndio mambo matano ya muhimu kuhusu kampuni ya Apple ambayo nimekuandalia kwa siku ya leo, bado kuna mambo mengi sana kuhusu kampuni hii hivyo kama unalo la kuongezea hakikisha unatumbia kwenye sehemu ya maoni hapo chini nasi tutaongeza kwenye makala hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use