Inawezekana ndio unaanza kutumia programu ya WhatsApp au hata pengine ulikua unatumia programu hiyo kwa miaka mingi sasa, lakini pia inawezekana ulikua unakosa kutumia programu hiyo vizuri kwa kutokujua mambo haya 10 yaliyopo kwenye programu hiyo maarufu ya WhatsApp.
- Kubadili Muandiko Kwenye Meseji
WhatsApp imefanikiwa kuongeza sehemu maalum ambazo zinakufanya kutumia programu hiyo vizuri na kwa urahisi zaidi. Kwa kuandika *maneno* utaweza kukoleza maandishi ya maneno kwenye meseji, kwa kuandika _maneno_ utaweza kuandika meseji kwenye staili ya mlazo na pia kwa kuandika ~maneno~ utaweza kuandika maneno na kuyawekea mkato. Bofya hapa kama unataka kujifunza njia hizi kwa video.
- Kurudia Meseji ya Mtu Kabla ya Kujibu (Quote)
Ili kuweza kurudia meseji ya mtu kabla ya kujibu shikilia meseji unayotaka kurudia kisha utaona imetokea menu yenye vitufe kazaa, kisha bofya kitufe cha nyota kisha utaona meseji ya mtu hyo imejiweka juu ya sehemu ya kujibu meseji, andika meseji yako kisha tuma.
- Kujua Unachati na Nani Sana (iPhone)
Kama unataka kujua unachati na nani sana na unatumia iphone njia hii ni rahisi sana. kwenye Whatsapp bofya Settings > Data and Storage Use > Storage Use hapo utaona majina yote ya watu uliochati nao sana bofya jina kuangalia idadi ya meseji picha au video ulizo chat na mwenzako. Kwa bahati mbaya kwa sasa bado hatuja weza kujua jinsi ya kufanya hivi kwenye simu za mfumo wa Android.
- Kujua Meseji Imefika na Kusomwa Saa Ngapi
Kama unataka kujua meseji uliyomtumia rafiki yako imefika na kusomwa saa ngapi, basi bofya kwenye meseji unayotaka kujua imefika sangapi kisha bofya kwenye sehemu iliyo na kitufe chenye alama ya (i) kisha utaona meseji yako imefika saa ngapi na kusomwa saa ngapi?
- Kuzima Sauti ya Mlio Kwenye Meseji za Mtu Mmoja (Mute Conversation)
Inawezekana uko busy na unataka kuzima sauti ya group au mtu mmoja pekee unaweza kufanya hivyo kwa kushikilia meseji ya mtu unae taka kuzima sauti ya meseji zake kisha bofya kwenye kona kisha bofya Mute.
- Kama Unataka Kuzima Last Seen
Kama unataka kuzima last seen kwenye programu ya WhatsApp fungua Settings > Account > Privacy > Last Seen. Kisha chagua unataka kuzima sehemu hiyo kwa watu gani, WhatsApp inakupa machaguo matatu ya kati ya : Everyone, My contacts, Nobody.
- Kuzima Tick Mbili za Blue za Kuonyesha Meseji Imefika
Kuna wakati utaki mtu asione kama umesoma meseji yake hivyo kama unataka kufanya hivyo unaweza kubofya Settings > Account > Privacy kisha ondoa tiki iliyoko kwenye maneno ya Read Receipts.
- Kuzuia WhatsApp kuifadhi Picha na Video Kwenye Simu (iPhone)
Kama unatumia iphone na hutaki kujaza simu yako kwa picha na Video zinazotumwa kwenye magroup mbambali basi unaweza kufanya hivyo kwenye programu hiyo kwa kubofya Settings > Chats kisha zima kwa kuchagua off kwenye sehemu iliyoandikwa Media.
- Hamisha Meseji Kwenda Kwenye Email
Kama unataka kuamisha meseji kwenda kwenye email fanya hivi, wakati unachati na mtu bofya More > Email Chat kisha hamisha meseji zako. Kumbuka njia hii ni kama unatumia simu yenye mfumo wa Android, Kama unatumia iPhone unaweza kuchagua jina la mtu unaetaka kuhamisha meseji zake kisha nenda mpaka mwisho utaona sehemu iliyoandikwa Export Chat bofya hapo na utanza kuamisha moja kwa moja.
- Kuficha Profile Picha Yako
Kama unataka kuficha profile picha yako kwenye programu ya whatsapp bofya Settings > Account > Privacy > Status kisha chagua My contacts only kisha hakikisha huja save namba ya mtu ambae hutaki aione profile picha yako.
Na hayo ndio baadhi ya mambo machache tu ambayo inawezakana kwa namna moja ama nyingine ulikua huyafahamu kwenye Programu ya WhatsApp. kama unataka kujifunza zaidi unaweza kutembea channel yetu ya Youtube Channel ili kujifunza zaidi kwa vitendo.
Ahsante
Asante sana Noi Noi kwa kutembelea Tanzania Tech.
nawap saluti wakubwa mnatisha
Asante sana na karibu
I love Tanzania nawapenda sana magufuli juu
Asante sana na karibu Tanzania Tech
Mungu awabariki sana kwa msaada huu wa kujua vitu vingine ambavyo sivijui
Asante sana Daudi